Brazil yawa Nchi ya Kwanza kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2018 Nchini Russia. - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, March 29, 2017

Brazil yawa Nchi ya Kwanza kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2018 Nchini Russia.

Timu ya Taifa ya  Brazil  imekuwa Nchi ya Kwanza kufuzu kwenda kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Nchini Russia huku wakiwa wamebakiza Mechi 4 za Kundi lao la Nchi 10 za Marekani ya Kusini.

Uhakika wa hili umetimia hii Leo March 29, 2017 baada ya Brazil kuwachapa Paraguay 3-0 na Uruguay kufungwa 2-1 na Peru katika Mechi ya mwisho iliyochezwa Alfajiri ya Leo.

Sasa Brazil wanaungana na Wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 -Russia ambao wamepitishwa moja kwa moja kucheza Fainali hizo.

Kwenye Kundi la Kanda ya Nchi za Marekani ya Kusini, Brazil walifungwa Mechi yao ya kwanza kabisa na Chile lakini baada ya hapo hawakufungwa tena katika Mechi zao 13 wakishinda Mechi 10 na Sare 3 wakivuna Pointi 33 wakifuatiwa na Colombia wenye Pointi 24.

Zikiwa zimebaki Mechi 4 kwa kila Timu, Timu nyingine ambazo zipo kwenye Nafasi za kufuzu moja kwa moja kwenda Russia ni Colombia, Uruguay na Chile.

Argentina, ambao wapo Nafasi ya 5, ikiwa watabaki Nafasi hiyo hadi mwishoni itabidi wacheze Mechi ya Mchujo na Nchi kutoka Kanda ya Oceania ili kufuzu kwenda Russia.

Jumatano Machi 29, 2017        

Ecuador 2 – 0  Colombia

Chile 3 – 1 Venezuela    

Brazil 3 – 0 Paraguay    

Peru 2 – 1 Uruguay

MSIMAMO.
 

Post Bottom Ad