Wakina Mama 580 wilayani Sengerema Wanufaika na mradi wa kutokomeza Vifo vya akina Mama na Watoto wachanga. - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, February 22, 2017

Wakina Mama 580 wilayani Sengerema Wanufaika na mradi wa kutokomeza Vifo vya akina Mama na Watoto wachanga.

Wakina mama zaidi ya 580 wilayani Sengerema wameweza kunufaika na mradi wa kutokomeza vifo vya akina mama na watoto wachanga. 

Mradi ulioanzishwa mwaka jana chini ya ufadhili wa Vodacom Foundation kwa ushirikiano na mashirika ya kimataifa ya USAID, Path Finder na Touch Foundation kugharamia mafunzoya afya na usafiri kwa akina mama wajawazito wanaokaribia kujifungua. 

 Vodacom Foundation inajuvunia kupata mafanikio makubwa katika kipindi kifupi na itaendelea kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha sekta ya afya nchini na kutokomeza vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga nchini.

Post Bottom Ad