VPL -2016/2017:Simba SC dole tupu..Ruvu Shooting yaibania Azam FC. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, February 11, 2017

VPL -2016/2017:Simba SC dole tupu..Ruvu Shooting yaibania Azam FC.

Wekundu wa Msimbazi Simba SC imerudi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Vodcom Tanzania Bara baada ya leo February 11,2017 kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons ya Mbeya,katika mchezo wa ligi hiyo uliochezwa  Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ushindi huo unaifanya Simba SC ifikishe pointi 51 baada ya kucheza mechi 22, ikiwashusha nafasi ya pili Mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 49 za mechi 21.

Katika Mechi ya Leo, Simba SC waliongoza 2-0 hadi Mapumziko kwa Bao za Juma Luizio na Ibrahim Ajib na lile bao la 3 Dakika ya 67 Mfungaji akiwa Laudit Mavugo.
Baada ya mchezo wa leo, Simba SC wanakwenda kujichimbia kujiandaa na mchezo dhidi ya mahasimu wao, Yanga SC Februari 25,2017 Uwanja wa Taifa.

Hapo kesho Jumapili,February 12,2017, zipo Mechi 3 za Ligi -VPL kwa Mwadui FC itacheza na Mbeya City kwenye Uwanja wa Mwadui wakati African Lyon itacheza na Mtibwa Sugar Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na pia JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Mbao FC kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
 

Post Bottom Ad