UEFA Europa League 2016/2017: Man United yasonga raundi ya 16 Bora. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, February 23, 2017

UEFA Europa League 2016/2017: Man United yasonga raundi ya 16 Bora.

Ndugu wa Paul Pogba wa Man United na Florentin Pogba wa St Etienne akivaa jezi maalum kuwa sapoti ndugu zake wote ambapo St Etienne wakiwa nyumbani wamejikuta wakikubali kipigo cha goli 1-0 na kuondolewa katika michuano ya Europa League kwa jumla ya goli 4-0 Katika mechi ya pili ya raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya UEFA Europa League na kusonga raundi ijayo .

Manchester United wameenda hatua ya 16 bora katika Ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League, kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Saint-Etienne.
 
Alhamisi iliyopita huko Old Trafford Man United waliichabanga Saint-Etienne 3-0 kwa bao za Hetitriki ya Zlatan Ibrahimovic.
Bao la ushindi la Man United lilifunbwa Dakika ya 16 kupitia Mkhitaryan alieunganisha Pasi ya Juan Mata.

Hata hivyo, mfungaji bao wao Henrikh Mkhitaryan huenda akakosa mechi ya Kombe la EFL Jumapili baada ya kuumia na kulazimika kuondoka uwanjani wakati wa mechi hiyo.

Muda mfupi baadaye hata hivyo, mchezaji huyo kutoka Armenia alionekana kuumia misuli ya paja na kulazimika kuondoka wuwanjani.

Beki wao Eric Bailly pia alifukuzwa uwanjani dakika ya 63 baada ya kuonesha kadi ya pili ya njano.

Jumatano Februari 22,2017.

Matokeo.

**Kwenye Mabano Jumla ya Magoli kwa Mechi 2

FC Schalke 04 1 PAOK Salonika 1 (4-1)

Fenerbahçe 1 FK Krasnodar 1 (1-2)

Saint-Étienne 0 Manchester United 1 (0-4)


Mechi za Pili

**Saa za Bongo

**Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza

Alhamisi Februari 23,2017.

1900 Osmanlispor v Olympiakos (0-0)

2100 Ajax v Legia Warsaw (0-0)

2100 Apoel Nicosia v Athletic Bilbao (2-3)

2100 Besiktas v Hapoel Be'er Sheva (3-1)

2100 Roma v Villarreal (4-0)

2100 Zenit St Petersburg v RSC Anderlecht (0-2)

2305 FC Copenhagen v Ludogorets Razgrad (2-1)

2305 Fiorentina v Borussia Mönchengladbach (1-0)

2305 KRC Genk v Astra Giurgiu (2-2)

2305 Lyon v AZ Alkmaar (4-1)

2305 Shaktar Donetsk v Celta Vigo (1-0)

2305 Sparta Prague v FC Rostov (0-4)

2305 Tottenham Hotspur v KAA Gent (0-1)

Post Bottom Ad