Taswira Picha,Dogo Janja Alizwa. - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, February 28, 2017

Taswira Picha,Dogo Janja Alizwa.

Msanii wa Bongo Fleva, Dogo Janja ameonekana kukosa raha baada ya gari yake kupata msala weekend hii iliyopita.

Dogo Janja amefunguka na kutuambia jinsi ilivyokuwa mpaka taa za mbele na nyuma na baadhi ya vifaa vya ndani ya gari yake kama radio kuibiwa… akizungumza na camera zetu msanii huyo alifunguka na kusema:

>> “Jana nilienda Moshi, nilikuwa na show ya Kili Marathon na baada ya kufanya show mchana usiku niligeuza kuja Dar es salaam, lakini inaonekana kuna watu walikuwa kwenye rader yangu wananifuatilia….“<<- Dogo Janja.

>> “… wamepiga power window, taa za mbele na za nyuma, na radio yaani wamepiga nyang’anyang’a. Asubuhi  naamka nimekuta gari inanizomea nilikuwa nahisi kama naota, nikawa nafikicha macho kuhakikisha…“<< – aliendelea kuelezea Dogo Janja.

Hizi ni baadhi ya picha za gari la Dogo Janja sasa.

Hitmaker huyo wa ‘Kidebe’ usiku wa kuamkia February 27,2017, ameibiwa baadhi ya vitu kwenye gari lake aina ya Porte ikiwemo taa, radio na power window. 

Baada ya kukutana na janga hilo Dogo Janja amemuandikia ujumbe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kupitia mtandao wa Instagram unaosemeka:

Muheshimiwa makonda tunashkuru umelisimamia vizur swala la madawa ya kulevya na tumeona matunda yake..lakin bado kuna hili la hawa wezi wa vipuli vya magari km taa radio powerwindow naona km alijaongelewa ivi..awa jamaa wapo wengi sana mjini na wanajulikana..wanakuibia alafu wanakupigia cm wapi pakuvipata vitu vyako..mueshimiwa tuanzishe na kampeni hii tupunguze kutiana hasara..kigali changu chenyewe ndio hiki nataftia riziki jana ucku wamekuja wameiba kila kitu radio taa za mbele na nyuma..ntatokaje kujitaftia rizik? Cc: @paulmakonda.


Post Bottom Ad