Sakata La Dawa za Kulevya:Freeman Mbowe arudishwa Polisi . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, February 21, 2017

Sakata La Dawa za Kulevya:Freeman Mbowe arudishwa Polisi .

Sakata la dawa za kulevya bado lipo kwenye vichwa vya habari Tanzania ambapo Jumatatu ya February 20,2017 imemuhusu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe aliyefika Polisi kwa mahojiano.

Jioni ya Jumatatu Mbunge huyo wa Hai, Kilimanjaro alichukuliwa na Polisi kwenye msafara wa magari yasiyopungua matatu ambapo iliripotiwa baadae kwamba Polisi walikwenda kufanya upekuzi kwenye nyumba zake Kawe na Mikocheni kwa mujibu wa Afisa habari wa CHADEMA.

Msemaji huyo wa CHADEMA,Tumaini Makene alithibitisha Polisi kupekua nyumba zake na kuandikisha maelezo ya majirani ambapo akasema kwenye mida ya saa sita usiku huu Polisi wamemrudisha Mbowe kwenye kituo cha Polisi kati na wamemfungulia jalada la Uchunguzi.

Siku ya Jumamosi,February 18,2017, Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro alimpa kiongozi huyo muda wa saa 48 za kujisalimisha vinginevyo watamtafuta kwa njia wanazozijua wao.

Mbowe aliitwa polisi kwaajili ya mahojiano kutokana na tuhuma za kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya pamoja na kulisababishia usumbufu na gharama jeshi la polisi.
                                                                                                                                          

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad