Picha:Msako wa Bangi Wakamata Wanne wilayani Ngara mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Thursday, February 23, 2017

Picha:Msako wa Bangi Wakamata Wanne wilayani Ngara mkoani Kagera.


Waliokamatwa Pichani ni Fabian Kasigo (45), mkazi wa Kazingati, Ndaluhekeye Chiza (37),Nestory Kachukuzi 42), Renatus James (44) Khalid John (33) wakazi wa wilaya ya Ngara ambapo Mkuu wa wilaya ya Ngara Luteni Kanali Michael Mtenjele alisema alisema wakulima waliokamatwa na kuhojiwa walidai wanauz zao hilo kati ya Sh15,000 hadi Sh 17 000 kwa wateja kutoka nchi jirani za Rwanda na Burundi na kwamba wanalima zao hilo wakikata miti kwenye vyanzo vya maji.

Pichani Bangi ndani ya Mahindi.

Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera ikiongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo Luteni Kanali Michael Mtenjele na iliwalazimu kuacha magari yao njiani na kutumia usafiri kwa pikipiki kuelekea kwenye mashamba ya kilimo cha bangi huko Kata ya Keza, tarafa ya Rulenge ambapo Jumla ya ekari 20 zimebainika na kukamatwa watu wanne wanaojihusisha na kilimo cha bangi katika mapori pamoja na misitu yaliyoko kitongoji cha Mulole kata hiyo ya Keza.Mkuu wa wilaya Ngara, Luteni Kanali Michael Mtenjele pichani kushoto sambamba na Katibu tawala wa Wilaya hiyo Vedastus Tibaijuka wakiipigwa butwaa kwenye shamba lililolimwa na kustawi Bangi katika Kata ya Keza,tarafa ya Rulenge.
Mkuu wa wilaya , Luteni Kanali Michael Mtenjele akifyeka Bangi  ambapo Jumla ya ekari 20 zimebainika na kukamatwa watu wanne wanaojihusisha na kilimo cha bangi katika mapori pamoja na misitu yaliyoko kitongoji cha Mulole kata hiyo ya Keza.
Mwenye chupa ya maji na sweta la bluu ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ngara Aidan Bahama ambapo alilazimika kutambaa akishuka na kupanda milima kuingia ndani ya mashamba ya bangi.

Picha na habari by Shaaban Ndyamukama
Post Bottom Ad