Mbowe agomea agizo la Makonda kwenda polisi, akanusha kujihusisha kwa vyovyote na dawa za kulevya. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, February 10, 2017

Mbowe agomea agizo la Makonda kwenda polisi, akanusha kujihusisha kwa vyovyote na dawa za kulevya.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema hatokwenda polisi kwaajili ya mahojiano kama alivyoitwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akilitaja jina lake kwenye orodha ya pili ya watu wanaohusishwa na biashara ya dawa za kulevya.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, Mbowe ambaye ni mbunge wa Hai, amesema Makonda hana amri ya kumpa wito mtu kwenda polisi kwa mujibu wa sheria ya serikali za mitaa.

Amedai kuwa mkuu wa huyo wa mkoa ‘amenichafulia jina langu, chama, familia na upinzani.’ “Sijawahi kufanya biashara ama kutumia madawa ya kulevya wakati wowote katika maisha yangu,” amesema Mbowe.

Mimi ni mtu mzima, ni kiongozi wa muda mrefu sijawahi kujihusisha kwa njia yoyote ama kuassociate na yeyote anayefanya biashara hiyo haramu ya madawa ya kulevya,” ameongeza.

Amedai kuwa licha ya kuunga mkono vita dhidi ya biashara ya madawa ya kulevya ambayo anaamini ilipaswa ianza zamani, lakini njia inayotumika ni ya hila na kinyume cha sheria.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad