Matokeo ya Hatua 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya. - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Thursday, February 23, 2017

Matokeo ya Hatua 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kasper Schmeichel alikuwa amecheza dakika 385 bila kufungwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ambapo Mechi ya marudiano itachezwa uwanja wa King Power tarehe 14 Machi,2017.

 Kipa wa Leicester, Kasper Schmeichel pia aliwafaa sana kwa kuokoa mkwaju wa penalti kutoka kwa Correa mabao yakiwa 0-0.
Hapo Jana  February 22,2017  usiku,ilichezwa michezo miwili ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2016/2017, kwa FC Porto walikuwa wenyeji wa Juventus katika mchezo uliomalizika kwa Juventus kupata ushindi wa goli 2-0 magoli yakifungwa na Marko Pjaca dakika ya 72 na Daniel Alves dakika ya 74.

Mchezo mwingine Sevilla walikuwa nyumbani kuwa kuikaribisha mabingwa wa Ligi Kuu England Leicester City katika mchezo huo wa kwanza wa hatua ya 16 bora, Sevilla walifanikiwa kuifunga Leicester goli 2-1, magoli yakifungwa na Pablo Sarabia dakika ya 25 na Joaquin Correa dakika ya 62 wakati goli la Leicester City likifungwa na Jamie Vardy aliyefunga goli hilo baada ya kucheza jumla ya dakika 748 bila kufunga goli.

Post Bottom Ad