Magonjwa ya Zinaa Yanayowapata Vijana - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, February 28, 2017

Magonjwa ya Zinaa Yanayowapata Vijana

KUNA magonjwa mengi ambayo watu hukumbana nayo lakini leo tutajadili magonjwa ya zinaa ambayo huwapa zaidi vijana japokuwa kuna wazee hukumbana nayo. 

Magonjwa haya huathiri sehemu za siri na huweza kusababisha muathirika kutopata mtoto Vijana wenye umri kati ya miaka 10 hadi 24 wako katika hatari zaidi ya maambukizi ya magonjwa hayo kwa kuwa wanapo balehe, hupata hisia au hamu ya kujamiiana.

 Hali hii husababishwa na vichocheo au homoni zilizomo mwilini zinazosababisha hisia za kufanya mapenzi.

Kuna aina mbalimbali za magonjwa ya zinaa ambayo yamegawanywa katika makundi kutokana na dalili zake.

KUNDI LA KWANZA

Kundi hili ni magonjwa yenye dalili za kutokwa usaha au majimaji sehemu za siri (ukeni na uumeni) ambayo ni kisonono, Trichomonas na Candida.

KUNDI LA PILI

Ni la magonjwa ya zinaa ambayo dalili zake ni kutokwa na vidonda, ambayo ni kaswende na malengelenge sehemu za siri. 

KUNDI LA TATU

 Hili ni magonjwa yenye dalili za kutokwa na uvimbe ambayo ni mitoki na pangusa sehemu za siri.

Mtu anaweza kuwa na zaidi ya ugonjwa mmoja wa zinaa kwa wakati mmoja. Kujitokeza dalili za ugonjwa wa zinaa hutegemea aina ya ugonjwa, jinsi na kinga ya mwili.

Hatari kubwa ya makundi yote ya magonjwa hayo ni kwa wanawake kwani asilimia 60 mpaka 70  (ya wanawake) wenye kisonono hawaoneshi dalili yoyote wakati wanaume ni kati ya asilimia 10 na 15. 

Hivyo ni muhimu kwa kijana wa kiume akiona dalili za ugonjwa kumueleza mwenzi wake wa kike aliyejamiiananaye ili wote waende kwenye kituo cha huduma ya afya kwa uchunguzi na tiba.

DALILI KWA MWANAMKE

Mwanamke aliyekumbwa na maambukizi ya ugonjwa wa zinaa mara nyingi hujisikia maumivu chini ya kitovu au kutokwa na usaha au majimaji yenye harufu mbaya sehemu za siri. 

Anaweza kuwashwa sehemu za siri au akatokwa na vidonda na vipele kwenye nyeti zake, mdomoni na sehemu nyingine za mwili.

Wakati wa kujamiiana anaweza kusikia maumivu au akawa amevimba mitoki, kuota mafindofindo sehemu za siri na kukojoa mara kwa mara kunakoambatana na muwasho au maumivu.

DALILI ZA UGONJWA WA ZINAA KWA WANAUME

Dalili za tatizo hili kwa wanaume ni kujisikia maumivu wakati wa kukojoa au kutokwa na usaha sehemu ya mbele kwenye dhakari. 

Mgonjwa atasikia maumivu makali sehemu za siri wakati wa kukojoa; atatokwa na usaha pamoja na kuwa na  vidonda sehemu za siri na mdomoni na atavimba mitoki na  kupata malengelenge sehemu za siri. Kwa ushauri  wasiliana na mtaalamu kwa namba za simu za hapo juu.


Post Bottom Ad