Listi nyingine ya FIFA/Coca Cola Ubora Duniani:Cameroon wapo nafasi ya 33 huku Tanzania ikishuka nafasi ya 158. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, February 10, 2017

Listi nyingine ya FIFA/Coca Cola Ubora Duniani:Cameroon wapo nafasi ya 33 huku Tanzania ikishuka nafasi ya 158.

Shirikisho la soka Ulimwenguni (FIFA) hapo jana February 09,2017 limetoa orodha mpya ya ubora wa viwango vya soka Duniani kwa nchi Wanachama , na Vinara wake bado ni Argentina wakifuatia Brazil na kwa Afrika ni Misri ndio wapo juu kabisa huku Tanzania ikishuka Nafasi 2 na kukamata Namba 158.

5 Bora kwenye orodha hiyo zimebaki zile zile bila mabadiliko na nazo ni Argentina (1), Brazil (2), Germany (3), Chile (4) na Belgium (5).

Kwa Afrika, Nchi ambayo iko juu kabisa ni Misri, waliotolewa Fainali ya AFCON 2017, ambao sasa wapo Nafasi ya 23 baada kupanda Nafasi 12 wakifuata Senegal walio Nafasi ya 31 na Mabingwa Wapya wa Afrika ambao ni Cameroon, wapo Nafasi ya 33 baada kupaa Nafasi 29.

Listi nyingine ya FIFA/Coca Cola Ubora Duniani itatolewa itatolewa Tarehe 9 Machi 2017.


Orodha hiyo ni;

  1. Argentina
  2. Brazil
  3. Germany
  4. Chile
  5. Belgium
  6. France
  7. Colombia
  8. Portugal
  9. Uruguay
  10. Spain
  11. Switzerland
  12. Wales
  13. England
  14. Poland
  15. Italy
  16. Croatia
  17. Mexico
  18. Peru
  19. Costa Rica
  20. Iceland
Kwa upande wa Afrika, Uganda bado wanaendelea kuongoza kwa Afrika Mashiriki wakiwa nafasi ya 17 kwa Afrika na 75 duniani wakifuatiwa na Kenya waliopo nafasi ya 20 Afrika na 87 duniani wakati Rwanda wako nafasi ya 27 Afrika na 100 duniani na Burundi nafasi ya 40 Afrika na 138 duniani.

Kwa upande wa Afrika, Misri wamekuwa vinara kwa kukwea kwa nafasi 12 na kutua kileleni wakiwa nafasi ya 23, wakifuatiwa na Senegal walioko nafasi ya 31 huku mabingwa wa michuano ya Mataifa ya Afrika Cameroon nao wakikwea kwa nafasi 29 mpaka nafasi ya 33 duniani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad