Happy Birthday YOUNG AFRICANS SC - 82th Anniversary. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, February 11, 2017

Happy Birthday YOUNG AFRICANS SC - 82th Anniversary.

Mabingwa wa Ligi kuu Tanzania bara mara 26 na Kagame Cup mara 5,Young Africans Leo February 11,2017 wanatimiza Miaka 82 toka kuanzishwa kwao 11. February, 1935.

Pamoja na kuendelea kupata Mafanikio katika Michezo ya Ligi Kuu Tanzania bara , Young Africans wameondoka Nchini leo Alfajiri  kuelekea visiwani Comoro kwa ajili ya mchezo wao wa klabu bingwa Afrika dhidi ya Ngaya Club siku ya Jumapili.

Young Africans  imesafri na Msafara wa wachezaji ishirini(20) benchi la ufundi nane( 8 )pamoja na viongozi wawili(2).

Wachezaji wanaoondoka ni.

Deogratius Munish, Ally Mustafa,Deud Kaseke,Haruna Niyonzima,Thaban Kamusoko, Amissi Tambwe, Mwinyi Haji, Saimon Msuva, Geoffrey Mwashuiya,Saidi Makapu, Hassan Ramadhani, Juma Mahadhi, Yusuph Mhilu, Obrey Chirwa, Nadir Haroub, Justine Zulu, Kelvin Yondani, Juma Abdul, Oscar Joshua na Emmanuel Martin.

Benchi la ufundi wanaoondoka ni.

George Lwandamina,Noel Mwandila,Edward Samwel Bavu,Juma Pondamali,Juma Zakaria Omary,Hafidhi Saleh Suleiman,Mohamed Omary Mwaliga na Jacob Sospeter Onyango.

Viongozi wanaosafiri.

Mussa Mohamed  Kisoki (TFF) na Paul Malume (Yanga Sc)

Baada ya kikosi kuwasili kinatarajiwa kufanya mazoezi yake leo jioni kwenye uwanja utakaochezewa mchezo siku ya jumapili.

Imetolewa na Idara ya Habari na mawasiliano.
Young Africans Sports Club
10.02.2017

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad