EPL-2016/2017: Arsenal 2-0 Hull- Sasa wako Nafasi ya 3 na Pointi 50. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, February 11, 2017

EPL-2016/2017: Arsenal 2-0 Hull- Sasa wako Nafasi ya 3 na Pointi 50.

Mchezaji Alexis Sanchez alifunga mara mbili na kuisaidia Timu yake ya Arsenal  kuishinda Hull City bao 2-0 katika mchezo wa Ligi kuu Uingereza leo February 11,2017 huku uamuzi wa refa ukidaiwa kuwa na utata.

 Arsenal walifunga Bao la Kwanza Dakika ya 34 baada ya Mpira kumgonga Mkononi na kutinga kufuatia kizaazaa cha Krosi Kieron Gibbs.
Bao la pili la Arsenal lilifungwa tena na Sanchez katika dakika za majeruhi, dakika ya 92, kwa Penati iliyotolewa baada ya Sam Clucas kuushika Mpira wa Kichwa wa Lucas Perez kwenye Mstari wa Goli.

Refa Mark Clattenburg aliwapa Penati Arsenal na kumpa Kadi Nyekundu Sam Clucas na Sanchez kufunga Penati hiyo.
Ushindi huo umewaweka Arsenal Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 50 sawa na Tottenham ambao wako Nafasi ya Pili lakini wanacheza baadae Leo huko Anfield na Liverpool.

Post Bottom Ad