Arsenal sasa usoni mwa Lincoln City robo fainali ya FA Cup. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, February 21, 2017

Arsenal sasa usoni mwa Lincoln City robo fainali ya FA Cup.

Usiku wa February 20,2017 timu ya Arsenal ilikuwa katika uwanja wa ugenini kucheza mchezo wake wa round ya tano ya FA Cup dhidi ya Sutton United inayoshiriki Ligi daraja la tano England, Sutton United na kuishinda kwa bao 2-0 ambapo ushindi wa Arsenal unaifanya kukutana na Lincoln City hatua ya robo fainali ya FA Cup.


Mchezo dhidi ya Sutton United haukuwa mwepesi sana kwa Arsenal, kwani licha ya kuutawala mchezo kwa asilimia 67 na Sutton wakitawala kwa asilimia 33, haikuisaidia Arsenal kupata ushindi wa idadi kubwa ya magoli na wameishia kupata ushindi 2-0 zilizofungwa na Lucas Perez dakika ya 27 na Theo Walcott dakika ya 55 ambapo hilo linakuwa goli lake la 100 toka ajiunge na Arsenal 2006.
Ratiba ya kombe hilo la FA katika hatua ya robo fainali sasa limeenda katika hatua ya raundi ya tano kwa  timu ya Manchester United inayoongozwa na Jose Mourinho ikipangiwa kukutana na Chelsea ya Antonio Conte katika hatua hiyo.

Man United imefanikiwa kuingia katika hatua hiyo baada ya kuifunga Blackburn Rovers 2-1 Jumapili  huku Chelsea wakiibuka kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wolves Hampton.

 Hii ni ratiba ya mechi za robo fainali ya kombe hilo ambapo zinatarajiwa kuchezwa kati ya Machi 11 na 12 ya mwaka huu.
                                
Chelsea vs Manchester United

Middlesbrough vs Huddersfield & Man City

Tottenham Hospurs vs Millwall

Lincoln City vs Arsenal

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad