Mapinduzi CUP 2017: January 10,Usiku Simba SC v Yanga SC…Azam FC v Taifa Jang’ombe. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, January 09, 2017

Mapinduzi CUP 2017: January 10,Usiku Simba SC v Yanga SC…Azam FC v Taifa Jang’ombe.

Watani wa jadi, Simba SC na Yanga SC watakutana Jumanne,January 10, 2017 Saa 2:15 usiku Uwanja wa Amaan, Zanzibar katika Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi 2017 visiwani Zanzibar.

Hiyo inafuatia Simba SC kushinda 2-0 dhidi ya Jang’ombe Boys jioni ya Jana January 08, 2017 katika mchezo wa mwisho wa Kundi A Kombe la Mapinduzi Uwanja wa Amaan.

Matokeo hayo yanaifanya Simba SC imalize kileleni mwa Kundi A kwa pointi zake 10, ikifuatiwa na Taifa Jang’ombe yenye pointi 9 .
Ikumbukwe ,Yanga  SC baada ya kusukumwa goli 4-0 na Azam FC kwenye mchezo wa January 07,2017, wakajikuta wanamaliza katika nafasi ya pili kwa pointi zao 6 nyuma ya Azam FC yenye pointi 7.

Kwa mujibu wa kanuni za mashindano, kinara wa kundi A anakutana na mshindi wa pili kutoka Kundi B wakati Kinara wa Kundi B yeye anakutana na timu iliyoshika nafasi ya pili katika Kundi A na hapo ndipo mechi ya Simba SC na Yanga SC inapozaliwa.

Hii ni mechi ya tano kwa watani wa jadi kwenye uwanja huo.
Taifa Jang’ombe ndio timu pekee kutoka Zanzibar ambayo imefuzu hatua ya nusu fainali ya kombe la Mapinduzi kwa mwaka 2017.

Taifa imefuzu baada ya ushindi wa goli 1-0 dhidi ya URA ya Uganda ambao ndio walikuwa mabingwa watetezi wa taji hilo. 

Bao la Mohamed Said ‘Messi wa Unguja’ limeifanya Taifa ifikishe pointi tisa pointi moja nyuma ya Simba ambao ni vinara wa Kundi A.
Mechi 2 fainali ya kombe la Kagame ambapo mwaka 1975 Yanga SC ilishinda 2-0, mwaka  1992 Simba SC ilishinda kwa penalti baada ya kutoka sare 1-1 . 

Simba SC ilishinda mechi ya ligi kuu 1-0 na fainali ya kombe la mapinduzi 2-0. 

Mechi hizo nne zinaonyesha Simba SC ikiwa na Historia ya kuifunga Yanga SC mara nyingi katika Uwanaja wa Amani. 

Hivyo basi tusubiri mchezo huo utakavyopigwa je Simba SC Historia itambeba au Yanga SC ndio itakuwa inafuta uteja ndani ya uwanj huu wa Amani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad