Yanga SC yachwapwa 2-0 na JKU ya Zanzibar kwenye Mchezo wa Kujipima Nguvu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, December 10, 2016

Yanga SC yachwapwa 2-0 na JKU ya Zanzibar kwenye Mchezo wa Kujipima Nguvu.

Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe akipiga mpira mbele ya kipa wa JKU, Mohamed Abrahaman leo Uwanja wa Uhuru.

Magoli mawili ya mchezaji  Emmanuel Martin  Kipindi cha Kwanza zimewapa Timu ya JKU ya Zanzibar ushindi wa mabao 2-0 walipocheza na Mabingwa wa Tanzania Bara Yanga SC katika Mechi ya Kirafiki Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam ikiwa ni Mechi ya kwanza kabisa chini ya Kocha kutoka Zambia George Lwandamina.

Lwandamina, aliechukua wadhifa huo Wiki mbili zilizopita kutoka kwa Mholanzi Hans van der Pluijm ambae amekuwa Mkurugenzi wa Ufundi hapo hapo Yanga SC.

Mzambia huyo, Leo alikuwa akisimamia Mechi yake ya kwanza na hilo lilionekana kwenye upangaji wa Timu kwani alijaribu kumpa nafasi kila Mchezaji.
Kipindi cha Pili, alibadili Wachezaji 10 kwa kuwaingiza Deogratius Munishi 'Dida', Juma Abdul, Mwinyi Hajji Mngwali, Vincent Bossou, Justin Zulu, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma, Simon Msuva, Amissi Tambwe na Deus Kaseke.

Licha ya kosa kosa kadhaa, Mabadiliko hayo hayakuwapa Yanga SC ,boa lolote.

Jumamosi ijayo Yanga watakuwa hapo hapo Uhuru-Katika mchezo wa Mechi za Mzunguko wa Pili.

Ligi Kuu Vodacom 2016/2017.

Mechi za Mzunguko wa Pili.

Ratiba

Jumamosi Desemba 17, 2016.

JKT Ruvu v Yanga [Uhuru Stadium, Dar es Salaam]

Mbeya City v Kagera Sugar [Sokoine, Mbeya]

Ruvu Shhoting v Mtibwa Sugar [Mabatini, Mlandizi]

Mwadui FC v Toto African [Mwadui Complex, Mwadui]
Jumapili Desemba 18, 2016.

Mbao FC v Stand United [CCM Kirumba, Mwanza]

Ndanda FC v Simba [Nangwanda, Mtwara]

African Lyon v Azam FC [Uhuru Stadium, Dar es Salaam]

Tanzania Prisons v Majimaji FC [Sokoine, Mbeya]

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad