Miaka 55 tangu Uhuru kutoka kwa Wakoloni mwaka 1961- Rais Magufuli ataja mambo yanayoikwamisha Tanzania. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, December 10, 2016

Miaka 55 tangu Uhuru kutoka kwa Wakoloni mwaka 1961- Rais Magufuli ataja mambo yanayoikwamisha Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzani Dr John Magufuli amesema sherehe za miaka 55 ya uhuru wa Tanganyika zimefanyika huku kukiwa na changamoto ya ukosefu wa ajira, upatikanaji wa huduma za jamii pamoja na rushwa.

Rais Magufuli amesema hayo wakati akiwahutubia watanzania katika sherere hizo ambazo zimefanyika Jana December 09,2016, katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam yaliyoongozwa na kauli mbiu isemayo “Kuunga mkono jitihada za kupinga Rushwa, Ufisadi na Kuimarisha uchumi wa viwanda kwa maendeleo yetu”.

Amesema jumla ya shilingi bilioni 29.5 ambazo zimetengwa katika bajeti ya mwaka huu,2016/2017, asilimia 40 ya fedha hiyo inatumika katika miradi ya maendeleo ili kuinua uchumi wa Tanzania.



 Akizungumza katika hotuba yake ya shukrani katika maadhimisho hayo ambayo yamefanyika katika uwanja wa uhuru jijini Dar es Salaam, Dkt. Magufuli, amesema kuwa serikali yake itaendelea kupambana na vitendo na rushwa na ufisadi, kwa ajili ya kuliletea taifa maendeleo.

Aidha Rais Dkt. Magufuli amesema kuwa serikali itahikisha kuwa inaondoa uonevu hasa kwa wananchi wanyonge ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili ili kila mtanzania aweze kufaidika na matunda ya nchi yake.

Maadhimisho hayo ambayo kwa mujibu wa Rais Magufuli ndio ya mwisho kufanyika Jijini Dar es Salaam na kuanzia mwakani ( 2017 ) yataadhimishwa Mjini Dodoma, yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali Wastaafu na Serikali pamoja na Mabalozi wa nchi mbalimbali zenye uwakilishi hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad