Halmashauri ya wilaya ya Ngara Mkoani Kagera yatoa msaada wa mabati 140 na kilo 42 za misumari kwa kaya 14 kati ya 39 zilizo ezuliwa na upepo - kijiji cha Kasulo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, December 09, 2016

Halmashauri ya wilaya ya Ngara Mkoani Kagera yatoa msaada wa mabati 140 na kilo 42 za misumari kwa kaya 14 kati ya 39 zilizo ezuliwa na upepo - kijiji cha Kasulo.

Mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera Luteni Kanali Michael Mtenjele ( kushoto ) sambamba na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Hiyo,Bw.Aidan Bahama ( Kulia ) wakiwa katika kijiji cha kasulo wilayani humo kwa ajili ya kugawa mabati katika kaya 14 kati ya 39 zilizo ezuliwa na upepo Novemba Mosi mwaka huu,2016.

Halmashauri ya wilaya ya Ngara Mkoani Kagera imetoa msaada wa mabati 140 na kilo 42 za misumari vyenye thamani ya shilingi milioni 1 laki Nane na elfu 48 kwa ajili ya kaya 14 kati ya 39 zilizo ezuliwa na upepo ulioambatana na mvua katika kijiji cha Kasulo Novemba mosi mwaka huu,2016.

Aidha baada ya Tathimini Kufanywa ya Uharibifu uliojitokeza,Jumla ya kaya 25 zilifanyiwa ukarabati wa kawaida huku kaya hizo 14 zikiharibika kwa kiwango kikubwa.
Luteni Kanali Michael Mtenjele akigawa mabati hayo,amepiga marufuku kwa wahusika kuuza vifaa hivyo kwa ajili ya kutafuta fedha ya kunywea pombe na kwamba atakayebainika hatua kali zitachukuliwa.

Amewahimiza kuyatumia kwa lengo lililokusudiwa ikiwa ni pamoja na  kujenga nyumba bora na imara  kwa kutumia tofari za kunyoma  ili kuepuka madhara kama yaliyotokea.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad