Na Mathias
Canal
Ndugu zangu
kama ambavyo tunakumbuka Tarehe 10/09/2016 majira ya saa 9 na dakika 27 Alasiri
maeneo ya Kanda ya ziwa hasa Mkoani Kagera kulitokea tetemeko la ardhi
linalokadiriwa kuwa na ukubwa wa 5.9 katika vipimo vya Richter ambapo Kitovu
cha tetemeko hilo ni kwenye makutano ya latitudo 10 06’ na longitudo 31055’
eneo ambalo ni kilomita 20 kaskazini mashariki mwa kijiji cha Nsunga na
kilomita 42 kaskazini magharibi mwa mji wa Bukoba na Kitovu hicho kilikuwa
kilomita 10 chini ya ardhi kwenye eneo hilo.
Tetemeko
hilo la ardhi liliacha familia kadhaa zikiwa na huzuni kubwa kwa kuwapoteza
ndugu, jamaa na rafiki zao ambapo idadi ya watu waliofariki walikuwa ni 17 huku
watu 560 wakipatiwa matibabu kutokana na majeraha waliyoyapata sambamba na
kukutikana kwa uharibifu wa makazi na miundombinu ya umma na watu binafsi.
Kwa Mujibu
wa Mtendaji Mkuu, Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) alieleza sababu za kutokea
kwa Tetemeko hilo la ardhi kuwa ilikuwa ni kutokana na kitovu cha tetemeko hilo
kuwa kiko chini sana ya ardhi (Km 10) na kwa kutafasiri umbile la mawimbi ya
tetemeko hilo yaliyonakiliwa na vituo vya kupimia matetemeko ya ardhi
inaonekana kuwa tetemeko hilo limetokana na misuguano ya mapange makubwa ya
ardhi iliyopasuliwa na mipasuko ya ardhi mithili ya mipasuko kwenye bonde la
ufa.
Kwa kuwa
eneo lililokumbwa na tetemeko la ardhi liko karibu na mkondo wa magharibi wa
bonde la ufa la Afrika Mashariki inakisiwa kuwa mtetemo huo ulisababishwa na
kuteleza na kusiguana kwa mapande ya miamba juu ya mipasuko ya ardhi ya bonde
hilo la ufa.
Katika siku
za karibuni kumekuwepo na taarifa mbalimbali katika mitandao ya kijamii ikiwemo
facebook, Twitter, Blogs, Instagram na Makundi mbalimbali ya Watsup jambo
ambalo lilinilazimu kufunga safari na kuweka kambi ya takribani siku nne Mkoani
Kagera ili kubaini ukweli wa namna fedha zilizopatikana na zilivyotumika ikiwa
ni pamoja na mahitaji mengine jinsi yalivyopatikana na namna yalivyoelekezwa.
UKWELI WA
MAMBO
Kufuatia
tathmini zilizofanyika kupitia wataalamu mbalimbali, makadirio ya awali
yalibaini kuwa kiasi cha jumla ya shilingi Bilioni 104.9 zinahitajika katika
kukabiliana na kurejesha hali katika Mkoa wa Kagera kufuatia maafa hayo. Ambapo
gharama hizi zinajumuisha:
a) Ujenzi wa
makazi ya muda kwa waathirika wa nyumba zipatazo 16,667 zilizoharibika katika
viwango tofauti, ambapo kiasi cha Shilingi Bilioni 41.7 zitahitajika.
b) Kiasi cha
shilingi 1.92 kwa ajili ya kodi ya miezi sita kwa wapangaji waliokuwa wakiishi
kwenye nyumba zilizoharibiwa.
c) Ukarabati
wa shule za msingi 163 kwa gharama ya shilingi Bilioni 12.7, sekondari 57 kwa
gharama ya shilingi Bilioni 45.65, vituo vya afya na zahanati 32 kwa gharama ya
shilingi milioni 772 na Majengo ya taasisi nyingine 20 kwa shilingi Bilioni 1.3
MISAADA
ILIYOTOLEWA
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu (WAZIRI MKUU NA
BUNGE) Ndg Uledi A. Mussa ilibainisha kuwa hadi kufikia Tarehe 13 Novemba, 2016
serikali ilikuwa imepokea misaada ya vifaa, Chakula, Fedha na ahadi mbalimbali
zenye thamani ya shilingi Bilioni 15.19 kutoka kwa wadau mbalimbali, washirika
wa Maendeleo, Balozi wan chi marafiki ambapo tayari misaada hiyo imeshagawiwa
na inaendelea kusambazwa kwa walengwa.
Msaada ya
misaada iliyopokelewa ni kama ifuatavyo:
v Fedha taslimu kiasi cha shilingi
Bilioni 5,412,934.82 kimeshapelekwa Benki.
v Kiasi cha shilingi milioni
17,579,427.00 kupitia mitandao ya simu
v Ahadi za shilingi Bilioni
6,703,000,000 Hivyo jumla ya ahadi na fedha taslimu hadi sasa ni Shilingi Bilioni
12,133,564,361.82
v Serikali pia imepokea misaada mingine
yenye thamani ya shilingi Bilioni 2.25 kama ifuatavyo: Unga Tani 58.12, Sukari
Mifuko 1,150, Mchele Tani 133.96, Maharagwe Tani 19.666. Mahindi Tani 70.1,
Majani ya Chai Tani 3, Maji Katoni 1,570, Mafuta lita 6,022, Sabuni Katoni 443,
Shuka 495, Blanketi 6,125, Vyandarua 2,821, Magodoro 1,146, Mahema 367 n
Turubai 6,237 vilipokelewa.
Aidha
serikali ilipokea vifaa vya ujenzi vikiwemo Saruji mifuko 24,433, Bati 20,933,
Misumari kilo 1475, Nondo vipande 725, Kofia za bati 150 na mbao 250.
Lakini
ifahamike kuwa baadhi ya waaliotoa ahadi kama serikali ya Uingereza wameahidi
kutekeleza ahadi zao kwa kujikita moja kwa moja katika ujenzi wa Shule, Mara
baada ya wakala wa majengo kuainisha viwango na gharama.
HATUA
ILIYOCHUKULIWA NA SERIKALI KATIKA KUKABILIANA NA MAAFA
Katika siku
za hivi karibuni kumekuwepo na juhudi za kujaribu kufanya upotoshaji kuhusu
hatua zilizochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa katika kukabiliana na maafa
haya, Ukweli ni kwamba serikali kwa kushirikiana na wadau imechukua hatua kubwa
za kuwasaidia waathirika ambapo miongoni mwao yafuatayo yameshafanyika:
Kutoa
matibabu bure kwa majeruhi wote 560, kuandaa na kugharamia mazishi ya watu 17
waliofariki ambapo Mheshimiwa Waziri Mkuu alihudhuria, Aidha serikali kwa
kushirikiana na wadau ilitoa mkono wa pole wa Shilingi Milioni 1.8 kwa kila
familia iliyopatwa na msiba.
Kuendelea
kutoa misaada mbalimbali ya kibindamu ikiwemo chakula, Madawa, Nguo, Makazi ya
muda, Huduma za tiba, Vifaa vya shule na huduma ya ushauri wa kisaikolojia kwa
waathirika katika Wilaya zote za Mkoa wa Kagera zilizopata athari.
Kushirikiana na Ofisi ya Mwakilishi Mkazi mmoja wa Mataifa na wadau mbalimbali
wakiwemo Msalaba Mwekundu, Plan International (T), BRAC (T), World Vision,
CARITAS, Save the Childre, JH Piego na Benki ya Dunia kufanya tathmini ya
pamoja ya mahitaji ya haraka ya athari za Tetemeko la ardhi ili kubaini maeneo
zaidi ya kuwasaidia wananchi.
HATUA ZA
KUREJESHA HALI
Tangu
kutokea kwa maafa haya serikali imeendelea kufanyia kazi masuala muhimu
yaliyoainishwa katika tathmini ya Tetemeko ambapo hadi kufikia tarehe 13
Novemba, 2016 licha ya kuendelea kuwapatia wananchi mahitaji muhimu kama
Chakula, Dawa na Misaada ya kujikimu katika makazi ya muda, kiasi cha shilingi
Milioni 969,238,326.35, Mifuko ya saruji 17,423, Bati 5,348 na Misumari Kilo
1,107 vilitumika kwa kufanya ukarabati mkubwa na mdogo wa shule za msingi na
Sekondari, Juhudi ambazo ziliwezesha wanafunzi wa shule hizo waliokuwa katika
hatari ya kukosa masomo kuendelea na masomo yao.
Gharama hizo
pia zimejumuisha ukarabati wa zahanati katika Halmashauri za Mkoa wa Kagera na kuanza
kwa ujenzi wa kituo kipya cha afya (Ishozi/Kabyaile) kitakachojumuisha chumba
cha upasuaji wa wodi ya kina mama na watoto kwa faida ya wananchi wote wa
maeneo hayo. Pia serikali imegharamia urejeshwaji wa miundombinu ya barabara,
maji na umeme katika maeneo kadhaa yaliyoathiriwa na tetemeko.
Shirika la
World Vision kwa kushirikiana na serikali mkoani Kagera, tayari limetoa jumla
ya mifuko ya saruji 2300 yenye thamani ya shilingi milioni 39,000,000 kwa kaya
460 zilizobomolewa nyumba na zilizoonekana kuwa na uhitaji zaidi ambapo katika
awamu ya kwanza kila kaya ilipaa mifuko mitano ya saruji na kwa sasa
utekelezaji wa awamu ya pili umeanza ambapo inatarajiwa kugawiwa mifuko ya
saruji 10,645 yenye thamani ya shilingi Milioni 164,997,000.00 kwa kaya 2,129.
Aidha tayari
serikali imeainisha kaya nyingine zilizoathirika zaidi zipatazo 370 za watu
waliomo kwenye makundi maalumu (Wazee, Wajane na Walemavu) ambao watapatiwa
vifaa vya ujenzi (Mabati 20 na mifuko 5 ya saruji kwa kila kaya) kwa ajili ya
kukarabati nyumba zao. Ugawaji kwa awamu ya kwanza umeanza.
HITIMISHO
Haya ndio
niliyoyabaini katika ziara yangu nilipozuru Mkoani Kagera naishauri Serikali
kuchukua hatua kali dhidi ya wale wate waliokuwa wanapotosha watanzania dhidi
ya matumizi ya fedha hizi kwa makusudi kwa madai kwamba zimeliwa na serikali.
Lakini
niwapongeze wananchi wote Mkoani Kagera ambao waliitikia wito wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuitikia wito wa kuanza ujenzi wa nyumba
zao wao wenyewe huku serikali ikiunga mkono katika maeneo baadhi kama ambavyo
nimeeleza katika makala yangu.
Jamii
inapaswa kutambua kuwa hakuna serikali duniani ambayo inapanga Tetemeko la
ardhi litokee ili liwauwe wananchi wake bali ni majanga ya asili ambayo kwa
namna moja ama nyingine hayazuiliki.
Kwa wale
wasomaji wa Biblia Takatifu Ukisoma Mathayo 3:2 inasema ”Tubuni, Kwa maana
ufalme wa mbinguni umekaribi” Nami nawasihi WATUBU wale wote waliokuwa
wanapotosha kuwa hela za rambi rambi zimeliwa tena walipotosha bila kuwa hata
na Data wala Taarifa sahihi za Matumizi ya fedha hizo.
Wakati
Mwema...!
|
No comments:
Post a Comment