Tazama Matukio Sita ya Udanganyifu yaliyotokea katika Mtihani wa Darasa la saba 2016 Nchini Tanzania. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, October 27, 2016

Tazama Matukio Sita ya Udanganyifu yaliyotokea katika Mtihani wa Darasa la saba 2016 Nchini Tanzania.

Akionyesha kaptula ya mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Tumaini iliyopo Wilaya ya Sengerema yenye majibu ya maswali ya mtihani wa Darasa la Saba iliyokamatwa.

Baraza la Mitihani la Taifa la Tanzania NECTA limetangaza Matokeo ya kumaliza Elimu ya Msingi ambapo kumekuwa na ongezeko la ufaulu kwa asilimia 2.52 kutoka asilimia 67.84 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 70.36 mwaka 2016.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa NECTA ,Dr Charles Msonde ameyasema hayo Leo Oktoba 27,2016  wakati anatangaza matokeo ya mtihani wa taifa wa Darasa la Saba kwa mwaka 2016.

Amesema watahiniwa 555,291 kati ya 789,479 waliofanya mtihani huo mwaka huu wamefaulu kwa daraja A, B, C, D na E na watajiunga na kidato cha kwanza mwaka 2017.

Kwa mujibu wa Dr Msonde, watahiniwa 238 wamefutiwa matokeo ya mtihani huo kutokana na udanganyifu ambapo shule sita, waalimu, wamiliki wa shule na wasimamizi wa mitihani wamebainika kufanya udanganyifu na kuwafanyia mtihani wanafunzi.
Kabla ya kutangaza matokeo hayo, katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Charles Msonde ameyazungumzia Matukio Sita ya udanganyifu yaliyotokea katika Mtihani wa Darasa la saba 2016.

1. Moja ya matukio ya udanganyifu ni pamoja na la  shule ya msingi Tumaini Sengerema ambapo mmiliki wa shule akishirikiana na wasimamizi alifanya mtihani na kuwapa majibu watahiniwa, wakayaandika kwenye sare zao wakaingia nayo kwenye chumba cha mtihani.

2. Shule ya little flower ambayo iko Serengeti, mwalimu mkuu akishirikiana na wasimamizi waliharibu mtihani wakaufanya na wakawapatia majibu wanafunzi, katika shule hiyo afisa wa baraza alipokuwa akifanya ufuatiliaji wa mitihani alimkamata mwalimu wa shule hiyo ambaye ni msimamizi akiwapa wanafunzi majibu.

3. Shule ya mihamakumi ambayo iko Sikonge mkoani Tabora, walimu walichukua form za kujibia mitihani, wanafunzi wanaingia chumba cha mtihani kutimiza wajibu tu baadae walimu wanachukua zile karatasi na kuanza kutoa majibu wao wenyewe

4.Shule ya Kashi Manyara, mwalimu alijificha chooni akiwa amepanga njama na mtahiniwa mmoja kwamba atoke na karatasi ya maswali ambapo mwalimu atafanya na baadaye mwanafunzi arudi chooni kuchukua majibu.

5. Shule ya St. Getrude Ruvuma, mwalimu mkuu na walimu kadhaa walifanya njama kuwaonyesha wanafunzi wote ambapo walipanga walimu wakae bwenini na kwenye nyumba ya mwalimu na wakaweka kikundi cha wanafunzi kadhaa ambao watakuwa wanapeleka maswali na baadae kuyaendea.

6. Shule kondi pamoja na kasandalala Sikonge watahiniwa walikuwa wote wanakosa kwa namna moja.

Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Charles Msonde amesema baraza la mitihani Tanzania limeshatoa taarifa ya walimu na wafanyakazi wengine waliokosa maadili na baraza hilo litafanya ufuatiliaji wa makusudi kwa wanfunzi waliofaulu hasa watakapochaguliwa sekondari kuona umahiri wao wa kuwawezesha kufaulu.

HAPA CHINI TAZAMA VIDEO ZAIDI KWA KUBOFYA KITUFE CHA KU PLAY.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad