Taswira 4 Ligi Kuu Uingereza 2016/2017:Chelsea 4-0 Manchester United. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, October 23, 2016

Taswira 4 Ligi Kuu Uingereza 2016/2017:Chelsea 4-0 Manchester United.

Chelsea imefanikiwa kuibutua bao 4-0 Manchester United leo hii Jumapili Oktoba 23,2016 katika moja ya mchezo mikali  wa Ligi kuu Soka nchini Uingereza msimu huu 2016/2017  huku mchezo huo ukirejesha  historia ya Jose Mourinho ndani ya uwanja wa Stamford Bridge tangu afukuzwe Umeneja Chelsea Desemba 2015.

Bao za Chelsea katika mchezo huu zimefungwa na Pedro dakika ya 1’’, Gary Cahill dakika ya 21’’, Eden Hazard dakika ya 62’’, N’golo Kante dakika ya 70’’.

Matokeo haya yamewaweka Chelsea Nafasi ya 4 wakati Manchester United wanabaki Nafasi ya 7.
Katika mchezo mwingine wa Leo, Manchester City wamerejea kileleni mwa  Ligi Kuu England, kufuatia  kutoka sare ya 1-1  dhidi ya Southampton kwenye Mechi iliyochezwa Etihad.

Matokeo haya yamewaweka Manchester City kwenye wimbi la Mechi 5 bila ya ushindi lakini wapo juu kwenye EPL kwa Ubora wa Magoli wakifungana kwa Pointi na Arsenal na Liverpool wote wakiwa na Pointi 20 kila mmoja baada ya Mechi 9.
EPL-OKT23

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad