Rais Magufuli na Neno lake Kuhusu Mikopo ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, October 21, 2016

Rais Magufuli na Neno lake Kuhusu Mikopo ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga tumba katika bendi ya Msondo Ngoma mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za wanafunzi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mke wake Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojiana Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandara wakipiga makofi wakati brass bendi ya JKT ilipokuwa ikitumbuiza mara baada ya kukamilika kwa tukio la kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za wanafunzi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono wakati akiwasili katika viwanja vya hosteli mpya za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Taaswira ya moja ya moja ya hosteli hizo za wanafunzi ambazo ujenzi wake umefikia asilimia 75 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu. 

PICHA NA IKULU.
Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema Serikali imetenga Shilingi Bilioni 483 kwa mwaka huu kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu ambapo wanafunzi zaidi ya 118,000 watanufaika.

Akizungumza katika uwekaji wa jiwe la msingi la hostel za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo,Oktoba 21,2016, Rais Magufuli amesema miongoni mwa hao watakaonufaika, wanafunzi 93,000 ni wanaoendelea na masomo na wanafunzi takribani 25,000 ni watakaoanza masomo mwaka huu huku akiweka bayana kuwa mikopo hiyo itatolewa kwa wanafunzi ambao wanatoka kwenye familia masikini.

Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kurekebisha dosari zilizopo katika mfumo wa utoaji wa mikopo ikiwa ni pamoja na upangaji mbaya wa wanafunzi katika vyuo, kutoa mikopo kwa upendeleo, kutozingatia sifa za mkopaji, kutoa mikopo hewa na kufungua vyuo kabla ya mikopo ya wanafunzi kutolewa na pia amewaonya wanafunzi kujiepusha na vitendo visivyofaa wakati Serikali inarekebisha dosari hizo.

"Na ndio maana wakati mwingine na wabaya wanapitia humo humo, mara fanye hivi fanyeni vile, wakati wanajua kuwa mkifanya yasiyofaa Serikali itawafukuza tu ili mkafanyie mambo yenu huko.

"Kwa sababu huwezi kuwa unahangaika kutafuta fedha za kuwapa mikopo, wakati huo huo unahitaji kujenga reli, wakati huo huo unahitaji kujenga barabara, wakati huo huo unahitaji kulipa mishahara, wakati huo huo unahitaji kutoa elimu bure, wakati huo huo Karagwe kuna njaa, wakati huo huo watu wanahitaji dawa hospitali, halafu watu wengine wanataka kukuendesha kana kwamba hela unayokusanya ni kwa ajili yao tu, ni lazima tuelewane na mimi ninataka kuwaeleza kwa dhati lazima twende katika njia iliyonyooka, ni bora uwe Rais usiye maarufu lakini utimize uliyoyaahidi, asitokee mtu wa kukuendesha, ninajua mmenielewa" amesisitiza Dkt. Magufuli.

Dkt. Magufuli ameiagiza Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) kujipanga vizuri kukusanya marejesho ya mikopo kwa wote waliokopeshwa na bodi hiyo ambapo mpaka sasa bodi inadai takribani Shilingi Trilioni 2.6.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad