Kamanda wa
Polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo
Na Woinde
Shizza,Monduli.
Jeshi la
mkoani Arusha linawashikilia watu Wa nne akiwemo mmiliki Wa Kambi ya LILAC inajishulisha
na maswala ya utalii mto Wa mbu John Kadozo(46) mwenye asili ya kiasia mkazi Wa
mto Wa mbu wilayani Monduli kwa kosa la kumchoma kwa kumwagia petroli
mfanyakazi wake.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo kamanda Wa Polisi mkoa Wa Arusha Charles Mkumbo alisema
kuwa tukio hilo lilitokea October 9 majira ya saa nne Usiku ndani ya Kambi ya
mtuhumiwa iliopo mto Wa mbu wilayani Monduli.
alisema kuwa
mtumiwa alimchoma moto mtoto aliyejulika kwa jina la Paskali Alfonce (17) mkazi
Wa mto Wa mbu aliyekuwa mpishi Wa
kampuni yake kwa kosa la kuchelewa kubandika maharage.
"Inasemakana
kijana huyu alikuwa mpishi Wa pale sasa Siku hiyo alipewa fedha akanunue
maharage alipoenda alichelewa kurudi ndipo mtuhumiwa na wenzake walipomkamata
kijana Huyo na kumwagia petroli kisha kumuwasha "alisema Mkumbo
Aliwataja
watuhumiwa wengine ambao walishirikiana kufanya tukio hilo na wote
wanashikiliwa na jeshi la polisi kuwa ni John Kadozo (46),George Kessy (28)
Martin Petro (16) Enock Wilium (19) na watuhumiwa wote wapo mahabusu na
wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mapema iwezekanavyo .
Akisimulia
tukio niko kwa uchungu mtoto Alfonce ambaye amelazwa katika hospitali
Seliani iliopo ngaramtoni alisema siku
hiyo alitumwa maharage ila alichelewa kurudi kutokana na kuyakosa lakini
aliporudi ndipo walipomkamata na kumfunga shuka mikono wakamwagia petroli kisha
kumchoma
"Nilibahatika
kuchoropoka nikakimbia sasa Jirani na hapo kuna mfereji nika rukia uko ndio
nikazimika maana niliwaka kabisa "alisema mtoto Alfonce
huku akilia
kwa uchungu.
Mama mlezi
aliyejitambulisha kwa jina la Cristina Faustine alisema anasikitika sana maana
amemlea huyo mtoto kwa shida tangu wazazi wake wafariki na aliamua amruhusu
kwenda kufanya kazi ili aweze kujikimu na aweze kujipatia maitaji yake.
Aidha alitumia
mud a huo kuiomba serekali kuakikisha mtoto uyo anapata matibabu na kwani
kwasasa anauwezo wakugaramia matibabu ya uyo mtoto.
|
No comments:
Post a Comment