Msimamo wa VPL baada ya matokeo ya mechi za leo October 22,2016. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, October 22, 2016

Msimamo wa VPL baada ya matokeo ya mechi za leo October 22,2016.

Yanga SC wameanza rasmi mbio za kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara – baada ya leo,Oktoba 22,2016  kuwatandika wenyeji Kagera Sugar mabao 6-2 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera.

Ushindi huo wa kwanza mkubwa zaidi msimu huu 2016/2017, unaifanya Yanga SC ifikishe pointi 21 baada ya kucheza mechi 10, ingawa inaendelea kukaa nafasi ya tatu nyuma ya Stand United yenye pointi 21 na Simba SC pointi 26. 

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Suleiman Kinugani aliyesaidiwa na Ferdinand Chacha na Nicholas Makalanga, Magoli ya Yanga SC yalifungwa na Donald Ngoma dakika ya 4, 73, Simon Msuva dakika ya 20, Obrey Chirwa dakika ya 25, 63 na Deus Kaseke, magoli pekee ya Kagera Sugar yalifungwa na  Mbaraka Yusuph aliyefunga magoli mawili dakika ya 3 na 48, hiyo ndio mara ya kwanza kwa uwanja wa Kaitaba kufungwa goli nyingi katika mechi za Ligi Kuu toka uwekwe nyasi bandia.

Matokeo ya Mechi nyingine za  VPL zilizochezwa Leo ni kama ifatavyo hapo chini.

Msimamo wa VPL baada ya matokeo ya mechi za leo October 22 2016, Azam FC vs JKT Ruvu watacheza saa 19:00.


Rekodi.

    Yanga SC imekuwa klabu ya kwanza msimu huu 2016/2017 wa Ligi kuu kufunga magoli mengi (6) katika mechi moja huku Kagera Sugar wao wakiweka rekodi ya kufungwa magoli mengi (6) katika mechi moja tangu kuanza kwa Ligi msimu huu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad