Msimamo wa Ligi Kuu-VPL 2016/2017 ulivyo kwa sasa baada ya Yanga kushinda 4-0 Leo Oktoba 26. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, October 26, 2016

Msimamo wa Ligi Kuu-VPL 2016/2017 ulivyo kwa sasa baada ya Yanga kushinda 4-0 Leo Oktoba 26.

Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara Yanga SC wameibuka na ushindi mnono wa mabao 4- 0 dhidi ya Ruvu JKT katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Goli la kwanza la Yanga SC lilifungwa na Obrey Chirwa   dakika ya 6 tu ya mchezo .

Kipindi cha pili dakika ya 62 dakika 6 toka aingie Amisi Tambwe aliivuruga safu ya ulinzi ya JKT Ruvu na kuipatia Yanga SC goli la pili.

Atajilaumu sana Maiko Aidani mlinzi wa JKT Ruvu kuruhusu mpira udunde mbele ya kipa wake na Amisi Tambwe kuiba mpira na kuutia kambani Hii ilikuwa dakika ya 90 likiwa goli la 4 na la mwisho.

Amisi Tambwe magoli haya mawili yamemfanya kufikisha magoli 60 toka atue nchini ndani ya ligi hii.

Tambwe kafunga magoli 19 akiwa na Simba SC na magoli 41 akiwa na Yanga SC .

Kwa sasa Tambwe anashika nafasi ya pili kwenye orodha ya wachezaji wanaoongoza kwa ufungaji –akiwa na magoli 6- nyuma ya nyota wa Simba aliye kwenye kiwango bora kwa sasa Shiza Kichuya mwenye magoli 7.
Kwa matokeo hayo,Yanga SC imefikisha pointi 24 kwenye msimamo wa ligi baada ya kucheza michezo 11 nyuma ya Vinara wa Ligi Simba SC wenye pointi 29 kileleni mwa ligi.

Mechi ijayo Yanga SC watacheza na Mbao FC jijini Dar.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad