Msimamo wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania 2016/2017 baada ya Matokeo ya Mchezo wa Leo Simba SC 1-0 MbaoFC. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, October 20, 2016

Msimamo wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania 2016/2017 baada ya Matokeo ya Mchezo wa Leo Simba SC 1-0 MbaoFC.

Bao pekee la mchezaji Muzamiru Yassin dakika ya 86 limeipa Simba SC pointi 3 nyingine kwenye uwanja wa Uhuru jiji Dar es Salaam Leo Oktoba 20,2016 wakati wakipambana na timu iliyopanda Ligi msimu huu Mbao FC kutoka jijini Mwanza.

Matokeo hayo yanaifanya Simba SC  iendelee kupaa kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbao FC ,ikifikisha pointi 26 baada ya kucheza 10 ikishinda nane na kutoa sare mbili – hivyo kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi sita zaidi.
Mchezo ujao wa Simba SC utakuwa dhidi ya Toto African ya Mwanza mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam wakati Mbao  FC wao watakuwa uwanja wa Sokoine kukabiliana na Tanzania Prisons.
Ushindi wa leo ni wa nane katika mechi 10 ambazo Simba SC wamecheza hadi sasa huku ukiwa ni ushindi wa tatu mfululizo wakiwa wametoka sare katika michezo miwili na kutopoteza mechi hata moja. 

(Simba SC 3-1 Ndanda FC, JKT Ruvu 0-0 Simba SC, Simba SC 2-1 Ruvu Shooting, Simba SC 2-0 Mtibwa Sugar, Azam 0-1 Simba SC, Simba SC 4-0 Majimaji, Yanga SC 1-1 Simba SC, Mbeya City 0-2 Simba SC, Simba SC 2-0 Kagera Sugar na Simba SC 1-0 Mbao FC).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad