Mongella:Utii wa Sheria za Usalama Barabarani Utasaidia juhudi za kupambana na Ajali kufanikiwa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, October 25, 2016

Mongella:Utii wa Sheria za Usalama Barabarani Utasaidia juhudi za kupambana na Ajali kufanikiwa.


Pichani juu ni maandamano ya bodaboda pamoja na wa watumiaji wengine wa barabara yakiingia Uwanjani kwenye maadhimisho hayo ambayo yamezinduliwa na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella.

Baada ya Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani kufanyika Kitaifa mkoani Geita kuanzia Septemba 29 hadi Oktoba Mosi Mwaka huu, Maadhimisho kama hayo kwa mkoa wa Mwanza yamezinduliwa hii leo kwenye Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza ambapo imeelezwa kwamba bado juhudi za kila mtumiaji wa barabara zinahitajika ili kutokomeza ajali za barabarani.

Kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani mkoani Mwanza, Robert Hussein, amebainisha kwamba kwa kipindi cha mwaka jana 2015, kati ya mwezi Januari na Septemba kulikuwa na ajali 161 zilizosababisha vifo 132 na majeruhi 187 na kwamba kwa kipindi kama hicho mwaka huu 2016 , kulikuwa na ajali 159 zilizosababisha vifo 150 na majeruhi 162 ambapo takwimu hizo zinaonesha kuwepo kwa ongezeko la vifo 18 sawa na asilimia 12 na upungufu wa majeruhi 25 sawa na asilimia 13.3
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, akizungumza kwenye uzinduzi wa wiki ya usalama barabarani mkoani Mwanza.

Kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani mkoani Mwanza, Robert Hussein, akizungumza kwenye uzinduzi wa wiki ya usalama barabarani mkoani Mwanza.

Na George Binagi-GB Pazzo

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, amewataka Watumiaji wa barabara mkoani Mwanza, kuzingatia sheria za usalama barabarani jambo ambalo litasaidia juhudi za kupambana na ajali kufanikiwa.

Mongella ametoa kauli hiyo hii Jana,Oktoba 24,2016, kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani mkoani Mwanza, uliofanyika katika Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza, ambapo elimu ya usalama barabarani itaendelea kutolewa kwenye maadhimisho hayo kwa juma zima.

Amesema watumiaji wote wa barabara wanao wajibu wa kufuata sheria za usalama barabarani huku akikemea tabia ya baadhi ya abiria wanaowahimiza madereva kuendesha vyombo vyao kwa mwendo kasi.


Akizungumza kwa niaba ya watumiaji wa barabara, Makamu Mwenyekiti wa Waendesha bodaboda mkoani Mwanza, Seifu Kagoma, amesema kila mtumiaji wa barabara anao wajibu wa kuwa na tahahadhali awapo barabarani badala ya kusubiri wajibu huo kutoka kwa mwenzake.

Maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani hufanyika kila mwaka nchini lengo likiwa ni kutoa elimu ya matumizi sahihi na salama ya barabara kwa makundi yote ya watumiaji wa barabara ambapo mwaka huu 2016 kitaifa yalifanyika mkoani Geita kuanzia Septemba 29 hadi Oktoba Mosi ambapo kauli mbiu yake ni “Hatutaki ajali, tunataka kuishi salama”.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad