Ligi Kuu Vodacom Tanzania 2016/2017 - Simba SC yatafuna 3-0 . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, October 23, 2016

Ligi Kuu Vodacom Tanzania 2016/2017 - Simba SC yatafuna 3-0 .

img_4669
Hatimaye ‘’Wekundu wa Msimbazi, Simba SC imefuta uteja kwa Toto Africans baada ya kuifunga bao 3-0 kwenye mchezo wa Ligi kuu soka Vodacom Tanzania bara msimu huu,katika mchezo huo wa leo Jumapili Oktoba 23,2016 kwenye uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.

Kabla ya mchezo wa leo, Simba SC ilikuwa haijawahi kutoka na pointi zote tatu katika mechi sita zilizopita kwa msimu uliopita Simba SC ililazimishwa sare ya goli 1-1 kwenye mchezo wa raundi ya kwanza CCM Kirumba lakini ikafungwa 1-0 kwenye mchezo wa marudiano.
img_4663
Ushindi wa leo (October 23, 2016), ni ushindi wa nne mfululizo kwa Simba SC huku ukiwa ni ushindi wao wa tisa katika mechi 11 walizocheza msimu huu 2016/2017 -hivyo kufikisha pointi 29 na sasa wanawazidi Mabingwa watetezi, Yanga SC walioa nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi nane,wakiwa na Pointi 21.
img_4627
Mchezo wa leo, Magoli ya Simba SC yamefungwa na Muzamiru Yassin ambaye alinza kuifunga goli la kwanza dakika ya 43 baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Fredick Blagnon.
img_4632
Laudit Mavugo aliyeingia kutoka benchi kuchukua nafasi ya Blagnon aliifungia Simba SC bao la pili dakika ya 52 akitumia vyema pasi ya Ibrahim Mohammed.
img_4656
Bao la tatu la Simba SC lilifungwa na Muzamiru Yassin dakika ya 74 na kuhitimisha ushindi uliokuwa ukisubiriwa na mashabiki wa Simba SC baata ya timu yao kucheza mechi nyingi bila ushindi mbele ya Toto Africans.
img_4618

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad