Ligi kuu Vodacom 2016/2017 – Matokeo Mechi za leo October 19 huku Yanga SC ikichapa Toto Africans 2-0. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, October 19, 2016

Ligi kuu Vodacom 2016/2017 – Matokeo Mechi za leo October 19 huku Yanga SC ikichapa Toto Africans 2-0.

Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Vodacom, Yanga SC  Leo hii Jumatano oktoba 19,2016 wameichapa Toto Africans  mabao 2-0 wakati wa mchezo huo wa Ligi kuu kwenye  CCM Kirumba Mwanza na  kwa ushindi huo kuwafanya wajichimbie nafasi ya Tatu.

Yanga SC sasa wana Pointi 18 kwa Mechi 9 wakitanguliwa na Stand United wenye Pointi 20 kwa Mechi 11 na kileleni wapo Simba  SC waliocheza Mechi 9 na wana Pointi 23.

Bao za Yanga  SC hii Leo zilifungwa kila Kipindi na Mzambia Obrey Chirwa na Penati ya Simon Msuva.

MSIMAMO VPL 2016/2017.
Kwenye Mechi nyingine hii Leo, huko Mlandizi Ruvu Shooting na Mwadui FC zilitoka 1-1 na ni matokeo ambayo pia yalitokea huko Nangwanda, Mtwara, Ndanda FC walipocheza na Mbeya City,na ngoma kuwa 1-1.

Huko Sokoine, Mbeya Tanzania Prisons iliinyuka Stand United Stand United 2-1 na kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam African Lyon ililala 2-0 toka kwa Maji Maji FC.

Mechi iliyobakia jii Leo ni ya huko Chamazi, Azam Complex, wakati Wenyeji Azam FC wakicheza na Mtibwa Sugar kwenye Mechi iliyoanza Saa 1 Usiku.

VPL itaendelea tena  kesho Alhamisi  Oktoba 20,2016 kwa Mechi  kati ya Simba SC na Mbao FC Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Ratiba/Matokeo.

Jumatano Oktoba 19,2016.

Azam FC v Mtibwa Sugar [Kuanza Saa 1 Usiku]

Ruvu Shooting 1 – 1 Mwadui FC 

Ndanda FC 1 – 1 Mbeya City 

Tanzania Prisons 2 – 1 Stand United 

Toto Africans 0 – 2 Yanga SC

African Lyon 0 -  2 Maji Maji FC

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad