LIGI KUU ENGLAND 2016/2017 – Wakati Arsenal Sare , Liverpool Yafunguka 2-1 sasa Wanakabana Kileleni kwa Pointi 20 wote. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, October 22, 2016

LIGI KUU ENGLAND 2016/2017 – Wakati Arsenal Sare , Liverpool Yafunguka 2-1 sasa Wanakabana Kileleni kwa Pointi 20 wote.


Pichani ni Mshambuliaji wa Timu ya Arsenal, Alexis Sanchez akisikitika kwa hasira baada ya kupoteza nafasi ya kufunga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu na wakilazimishwa sare ya 0-0 na Middlesbrough  leo oktoba 22,2016 Uwanjani Emirates, London.

Matokeo hayo yamemaliza wimbi la ushindi wa Mechi 6 mfululizo lakini yamewapa  Pointi 1 na kufikisha alama 20. Timu ya Pili ni Liverpool walioshinda 2-1 dhidi ya West Brom na Pointi zao 20 wakitofautiana magoli na Arsenal huku Manchester City ambayo Kesho,Jumapili Oktoba 23,2016 ipo kwao Etihad kucheza na Southampton na ushindi au Sare itawarejesha kileleni kwani wana Pointi 19.
Kwenye Mechi nyingine za Leo, Bao la dakika ya 90 la Scott Arfield liliwapa Burnley ushindi wa 2-1 dhidi ya Everton waliotawala Mechi hii.

Nao Mabingwa Watetezi Leicester City, wakiwa kwao King Power Stadium, waliitandika Crystal Palace 3-1 kwa Bao za Ahmed Musa, Shinji Okazaki na Christian Fuchs huku Palace wakifunga kupitia Yohan Cabaye.

Matokeo Mengine kama yanavyoonekana hapa chini.

EPL - LIGI KUU ENGLAND 2016/2017.

Jumapili Oktoba 23,2016.

1530 Man City v Southampton  
 
1800 Chelsea v Man United

LIGI KUU ENGLAND 2016/2017 MSIMAMO BAADA YA MECHI ZA LEO.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad