Ifahamu CV ya Kocha George Lwandamina wa Yanga SC akisaini Miaka Miwili. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, October 25, 2016

Ifahamu CV ya Kocha George Lwandamina wa Yanga SC akisaini Miaka Miwili.

Kocha George Lwandamina mwenye umri wa miaka 53 alizaliwa mwaka 1963 Mufulira nchini Zambia akisimama kama mmoja wa magwiji wa soka nchini humo na Afrika kwa ujumla kutokana na historia yake nzuri toka akiwa mchezaji na baadae kocha.

Lwandamina akiwa kama mchezaji aliweza kuimudu vyema nafasi ya mlinzi wa kati. Alianza kusikika katika soka baada ya mwaka 1984 kujiunga na timu ya Mutondo Stars na akisimama kama beki wa kati wa kutumainiwa hali iliyomfanya kuitwa timu ya taifa ya Zambia . 

Alidumu na timu hiyo kwa msimu mmoja tu kabla ya kutimkia timu ya Mufulira ikiwa timu ya nyumbani kwao na hii ni baada ya ushawishi mkubwa wa viongozi wa timu hiyo.

Alidumu na Mufulira mpaka january 17, 1989 alipoamua kuachana na timu hiyo. alianza mafunzo ya ukocha huku akichezea timu mbalimbali lakini si ngazi ya ushindani . 

Baada ya kumaliza mafunzo yake 1997 alirudi Mufulira kama kocha mkuu. Hii ni Mufulira wanderers tofauti na ile Mufulira blackpool , Timu pinzani katika mkoa wa Mufulira.

Aliachana na Mufulira mwaka 2000 baada ya kuwawezesha kuwa mabingwa wa ligi kuu na kutimkia Green Buffaloes aliyoifundisa toka mwaka 2002 hadi mwaka 2009 lakini hakuwahi kuipa kombe lolote zaidi ya kucheza fainali ya Chibuku mwaka 2005 na kushindwa.

2009 mpaka 2010 alijiunga na Kabwe Warriors timu ambayo aliiwezesha kuwa moto wa kuotea mbali nchini Zambia na hawa ndio waliomfanya gwiji huyu kupendekezwa na mkongwe Kalusha Bwalya kuinoa timu ya taifa ya Zambia al maarufu kama Chipolopolo ( risasi za shaba ).

2011 hadi 2014 alijiunga na Red Arrows akiipa ubingwa wa kombe la Barclays mwaka 2013 na mwaka 2014-15 kuchaguliwa kocha bora nchini Zambia . 

Mafanikio na Red Arrows yaliwafanya mabosi wa Zesco United kumnyakua mwaka 2014 na kuwawezesha kuwa mabingwa wa ligi 2014 na 2015 mara mbili mfululizo katika ligi yao maarufu sana kwa jina la ZAMBIAN SUPER LEAGUE ikiwa ligi ya pili kwa ubora kusini mwa Afrika baada ya ligi kuu nchini Afrika Kusini.

Mwaka huohuo wa 2014pia aliwawezesha Zesco United kunyakua kombe la Barclays . 

Hii ilimfanya kumpa heshima kubwa nchini humo kwa msimu wa kwanza kuchukua kombe la ligi kuu na kombe hili la Barclays .

Huyo ndio George Lwandamina kocha mkuu wa timu ya taifa ya Zambia pia bado ana kandarasi ya miaka miwili na Zesco United inayoisha February 17 2017. 

Mabosi wa Yanga SC wamemleta nchini kuchukua nafasi ya Hans Van Pluijm na tayari amelamba kandarasi ya miaka miwili.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad