Taswira Picha ya Kombe Kili Queens..Hongereni Wanawake wa Tanzania”. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, September 21, 2016

Taswira Picha ya Kombe Kili Queens..Hongereni Wanawake wa Tanzania”.

Kombe hili limechukuliwa na Timu ya soka ya Wanawake ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens jana Septemba 20,2016 ilipotawazwa kuwa Mabingwa wa kwanza Kombe la Chalenji 2016 kwa nchi za Afrika Mashariki na kati baada ya kuifunga Kenya mabao 2-1.

Michuano hiyo iliyofanyika Jinja Uganda imeanzishwa kwa mara ya kwanza na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Mashujaa wa Kili Queens jana walikuwa Mwanahamisi Omary na Stumai Abdallah waliofunga mabao hayo kabla ya mapumziko.

Michuano hiyo ilishirikisha timu 11 ambapo Tanzania katika safari yake iliifunga Rwanda ikatoka sare ya bila kufungana na Ethiopia kabla ya kuwafunga wenyeji Uganda kwenye mechi ya nusu fainali.

Timu nyingine zilizoshiriki michuano hiyo ni Zanzibar, ‘Zanzibar Queens, Burundi na Ethiopia. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad