Rais Magufuli atengua uteuzi wa RAS Kagera na DED Manispaa Bukoba. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, September 27, 2016

Rais Magufuli atengua uteuzi wa RAS Kagera na DED Manispaa Bukoba.

Aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Amantius Msole.

Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli ametengua uteuzi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Bw.Amantius Msole na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Bw.Steven Makonda baada ya kubaini kuwa wamefungua akaunti nyingine ya benki kwa kutumia jina linalofanana na akaunti rasmi ya kuchangia maafa iitwayo "Kamati Maafa Kagera" kwa lengo la kujipatia fedha.

Kwa mujibu wa Ikulu jijini Dar es Salaam ,taarifa iliyotolewa leo September 27,2016 na Waziri Mkuu, Bw.Kassim Majaliwa muda mfupi baada ya kupokea hundi ya msaada kutoka kwa Waziri Mkuu wa India, Mhe.Narendra Modi iimeeleza kuwa pamoja na kutengua uteuzi huo Rais Magufuli ameagiza vyombo vya dola vichukue hatua dhidi ya wote waliohusika katika njama za kufungua akaunti hiyo. 

Msaada huo ni wa shilingi Milioni 545.

Aidha, Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Simbaufoo Swai kutokana na kuhusika katika njama hizo.

Hata hivyo Waziri Mkuu ametoa wito kwa wananchi na taasisi mbalimbali kuendelea kuchangia misaada kwa ajili ya walioathirika kwa kutumia akaunti rasmi ya "Kamati Maafa Kagera" ambayo imetangazwa na Serikali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad