Ligi ya Mabingwa barani Ulaya 2016/2017- Msimamo wa Kundi A -D baada ya Mechi za Septemba 28,2016. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, September 29, 2016

Ligi ya Mabingwa barani Ulaya 2016/2017- Msimamo wa Kundi A -D baada ya Mechi za Septemba 28,2016.

Ligi ya Mabingwa barani Ulaya imeendelea tena Usiku wa Jana Septemba 28,2016 katika hatua ya makundi ambapo CELTIC imetibua kasi ya Manchester City baada ya kulazimisha sare ya 3-3 kwenye mchezo ulichezwa Celtic Park. 

Manchester City kama wangeshinda mchezo huu wa 11 mfululizo kwenye mashindano yote, wangefikia rekodi ya England iliyowekwa na Tottenham mwaka 1960.

Bao za Man City zimefungwa na Fernandinho dakika ya 12'', Raheem Sterling dakika ya 28'', na Nolito dakika ya 55'' huku za Celtic zikifungwa na Moussa Dembele dakika ya 3'', 47 na 20 kwa Man City kujifunga.
Yannick-Ferreira Carrasco akifunga kwa bao safi la shuti la chini na kumpita kipa wa Bayern Munich goalkeeper Manuel Neuer.

Atletico Madrid imepiga hatua kubwa kuelekea 16 bora ya Ligi ya Mabingwa baada ya kuwafunga mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich 1-0 kwenye uwanja wa Vicente Calderon. 

Bao hilo pekee la Atletico Madrid lilifungwa na Yannick-Ferreira Carrasco kunako dakika ya 35.
Matokeo ya mechi zote zilizochezwa Jumanne usiku,Septemba 27,2016 ni kama ifuatavyo: 

Champions League - Group E 

CSKA Moscow 0 - 1 Tottenham Hotspur 

Monaco 1 - 1 Bayer Leverkusen 

Champions League - Group F 

Borussia Dortmund 2 - 2 Real Madrid 

Sporting CP 2 - 0 Legia Warszawa 

Champions League - Group G 

FC Koebenhavn 4 - 0 Club Brugge 

Leicester City 1 - 0 FC Porto 

Champions League - Group H 

Dinamo Zagreb 0 - 4 Juventus 

Sevilla 1 - 0 Lyon

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad