Ligi Kuu Uingereza 2016/2017-Arsenal waikalisha 3-0 Chelsea. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, September 24, 2016

Ligi Kuu Uingereza 2016/2017-Arsenal waikalisha 3-0 Chelsea.


Wachezaji wa Arsenal wakifurahia ushindi wao wa nyumbani  Emirates Jijini London , Arsenal wameiadhibu Chelsea mabao 3-0 kwenye Mechi ya Ligi Kuu Uingereza kwa mabao yao kufungwa na Alexis Sanchez, Theo Walcott na Mesut Ozil.

Kwenye EPL tangu Arsenal wafungwe 4-3 na Liverpool kwenye Mechi ya kwanza ya Msimu na kisha kutoka 0-0 na Mabingwa Leicester, Arsenal wameshinda Mechi zao zote 3 zilizofuatia kwa kuzichapa Watford 3-1, Southampton 2-1 na Hull City 4-1.

Katika Mechi zao 2 zilizopita za Ligi, Chelsea walitoka Sare na Swansea na kisha kufungwa na Liverpool .

Bao hizo 3 zilisimama hadi Mpira kwisha na kuwasimika Arsenal Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 1 nyuma ya Tottenham na 5 nyuma ya Vinara Man City.

Kwa Chelsea hiki ni kipigo cha Pili mfululizo kwenye EPL baada ya pia kuchapwa na Liverpool 2-1 na sasa wameshuka hadi Nafasi ya 8.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad