Ligi Kuu Vodacom 2016/2017 - Wapigadebe wa Shinyanga wavunja rekodi ya Yanga SC kwa ushindi wa bao 1-0. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, September 26, 2016

Ligi Kuu Vodacom 2016/2017 - Wapigadebe wa Shinyanga wavunja rekodi ya Yanga SC kwa ushindi wa bao 1-0.


Timu ya Stand United ‘Chama la Wana’ wamevunja rekodi ya Yanga SC baada ya kuifunga bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa Jana September 24,2016 kwenye uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga.

Bao pekee la Stand United limefungwa na Pastore Athanasi Dakika ya 58’’ambalo limeifanya timu take iibuke na pointi tatu kwenye uwanja wa nyumbani na umewainua Stand United hadi Nafasi ya Pili wakiwa na Pointi 12 zikiwa ni Pointi 2 nyuma ya Vinara Simba wenye Pointi 16 huku wote wakiwa wamecheza Mechi 6 kila mmoja.

Mechi inayofuata kwa Mabingwa Yanga SC ni Dabi ya Kariakoo dhidi ya Mahasimu wao Simba SC hapo Jumamosi Oktoba Mosi,2016 ndani ya Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na Timu hiyo inatarajia kung’oka Shinyanga kwenda Visiwani Pemba kujipanga upya kwa kitimitim chao na Vinara Simba SC.

Ratiba/Matokeo VPL 2016/2017.


Jumatatu Septemba 26,2016.


African Lyon v Kagera Sugar

Jumamosi Septemba 24,2016.

Simba 4 – 0 Majimaji FC

Tanzania Prisons 0 – 0 Mwadui FC

Mtibwa Sugar 1 – 1 Mbao FC

JKT Ruvu 2 – 0 Mbeya City

Ndanda FC 2 – 1 Azam FC

Licha ya Stand United kuwa kwenye mpasuko mkubwa wa kiutawala, timu hiyo bado haijapoteza mchezo wowote hadi sasa tangu kuanza kwa ligi mzimu huu 2016-2017.

Stand United meshinda mechi tatu na kutoka sare kwenye michezo mitatu. (Stand UTD  0-0 Mbao FC, Kagera Sugar 0-0 Stand UTD, Stand UTD 1-0 Toto Africans, Mwadui FC 2-2 Stand UTD, Stand UTD 2-1 Ruvu JKT, Stand UTD 1-0 Yanga)

Rekodi za Yanga zilizo vunjwa na Stand United

    Stand United imeifunga Yanga SC kwa mara ya kwanza tangu timu hiyo ya Shinyanga mjini ilipopanda daraja.

    Yanga SC imepoteza mchezo wake wa kwanza wa  VPL msimu baada ya kucheza mechi nne bila kufungwa. 

Mara ya mwisho Yanga SC kupoteza mechi ilikuwa 3-1 dhidi ya TP Mazembe nchini DR Congo katika mashindano ya kombe la shirikisho barani Afrika hatua ya makundi.

    Stand United imekuwa timu ya kwanza kufunga goli dhidi ya Yanga SC. Awali Yanga SC ilikuwa imecheza mechi nne za ligi bila kuruhusu goli huku yenyewe ikiwa imefunga magoli nane. 

(Yanga 3-0 African Lyon, Ndanda 0-0 Yanga, Yanga 3-0 Maji Maji, Mwadui 0-2 Yanga).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad