Magari 36 ya Mizigo Kutoka Tanzania kwenda Burundi yasitisha Huduma kituo cha Forodha Kobero. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, August 26, 2016

Magari 36 ya Mizigo Kutoka Tanzania kwenda Burundi yasitisha Huduma kituo cha Forodha Kobero.


Madera wa Tanzania wanaoendesha magari ya mizigo kuingia nchini Burundi wamejikuta katika wakati mugumu baada ya kunyanyaswa na askari wa burundi kwa kuwatoza fedha zisizokuwa na stakabadhi ambapo fedha zinapokosekana wanafungiwa  kwenye vyoo.

 Mmoja wa madereva wa magari hayo Bw Maskini Juma amesema askari wa burundi katika kituo cha forodha Kobero nchini humo walimfungia chooni saa 18 wakitaka shilingi au faranga laki 4 huku wakiwa amefanya kosa la kukutwa akiongea na mwana mke ndani ya gari.

Aidha dreva mwingine aliyepigwa shaaban Juma amesema madereva wamekaa  kobero mwezi mmoja na nusu  wakipeleka chakula cha shirika la cartas nchini Burundi lakini hawajaruhusiwa kuingia nchini humo kwa kukosa vibali



Hata hivyo  kiongozi wa Jeshi la polisi katika mkoa wa muyinga Kabul Jamali  amesema changamoto za usalama na mazingira wanazolalamikia madereva wa Tanzania yatashughulikiwa kuimarisha mahusiano mema baina ya Tanzania na Burundi



Katika hatua hatua nyingine viongozi wa usalama upande wa kata ya kabanga wilayani ngara  wamewahimiza madereva kusitisha mgomo wa kuendelea na safari na kuutaka uongozi wa burundi kuondoa vikwazo  ili amani iweze  kupatikana.

HABARI/PICHA:-Shaaban Ndyamukama-Ngara,Kagera.




Baada ya majadiliano ya muda mrefu wa viongozi wa pande mbili za mpakani, Kamanda wa Jeshi la Polisi wa mkoa wa Muyinga nchini Burundi, Kabura Jamali ( katikati Pichani ) anayesimamia askari wa Kobero, aliahidi kuwachukulia hatua na kuwasihi madereva kuendelea na safari zao hadi Bujumbura na mikoa mingine ya nchi hiyo.




Dereva juu na chini Shaaban Juma Mohamed yeye alikamatwa na askari polisi wa Burundi,baada ya kukamata kijana aliyekuwa akichana tulubali la gari lake kuiba mfuko wa ngano na mapigano yalianza baina ya kijana huyo na tingo wa gari lake naye katika kuwaamua, ndipo alishambuliwa na askari wa Burundi mgongoni na mguuni.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad