UHALIFU NGARA:-* Watu wanaodhaniwa kuwa Majambazi wavamia kijiji cha Mabawe ,Waua kisha kupora Mali Dukani. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, July 28, 2016

UHALIFU NGARA:-* Watu wanaodhaniwa kuwa Majambazi wavamia kijiji cha Mabawe ,Waua kisha kupora Mali Dukani.

Muonekano kwa mbali wa Barabara kuu inayounganisha Nchi ya Burundi na wilaya ya -Ngara mkoani Kagera - ambayo imekuwa ni msaada mkubwa sana kwa Wananchi wa nchi za Tanzania,Rwanda na Burundi kuitumia katika shughuli za  usafirishaji.

Watu wanaodhaniwa kuwa Majambazi wamevamia kijiji cha Mabawe wilayani Ngara mkoani Kagera na kumuua mkazi wa kijiji hicho kisha kupora Mali dukani kwake na kukimbia wakielekea nchini Burundi.

 Mtendaji wa kijiji hicho Bw Joseph Festo amemtaja aliyeuawa kuwa ni Joseph Maganga mwenye umri wa miaka 24 na kwamba majambazi hao walimtaka kijana huyo awape fedha na wakati wa mabishano walimpiga risasi na kufariki papo hapo ambapo Mwili wake umehifadhiwa kwenye Kituo cha afya cha Mabawe

Amesema katika tukio hilo lililotokea Jana July 27,2016,majira ya Usiku, Mwanafunzi Nice Mathias anayesoma Darasa la 7 katika Shule ya msingi Mabawe amejeruhiwa mguuni kwa kupigwa risasi na majambazi hao wakati wakibishana na mwenye duka baada ya kwenda kushuhudia ubishi huo

Mkuu wa Jeshi la polisi wilayani Ngara Bw Abel Maige amethibitisha tukio hilo na kwamba mtu mmoja anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuwasafirisha wahalifu kwa pikipiki kuelekea mpakani mwa nchi jirani ya Burundi.HABARI NA RADIO KWIZERA FM.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad