Baraza linapenda kutoa taarifa kuwa
Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) umefunguliwa tena kuanzia tarehe 22 Julai 2016
ili kujaza nafasi za udahili zilizo wazi baada ya Baraza kuchagua waombaji
udahili waliowasilisha maombi yao kuanzia tarehe 4 Machi 2016 hadi tarehe 3
Juni 2016. Mwisho wa kuwasilisha maombi ni tarehe 5 Agosti 2016 saa sita
usiku.
Waombaji wapya na baadhi ya waombaji
walioshindwa kukamilisha maombi yao kupitia mtandao ilipofika tarehe 3 Juni
2016, wanaarifiwa kuanza kuwasilisha maombi ya udahili kupitia Mfumo wa Udahili
wa Pamoja (CAS) ili kujaza nafasi zilizo wazi. Waombaji wanahimizwa kutumia
muda huu wa nyongeza ili kuwasilisha maombi.
Baraza linapenda pia kuwaarifu
waombaji udahili na umma kwa ujumla kuwa vikao vya Kamati za kuidhinisha majina
ya waombaji udahili kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) vilipitisha orodha
ya majina ya wenye sifa za udahili kulingana na nafasi za udahili kwa
kila kozi zitolewazo na vyuo husika kati ya tarehe 18 Julai 2016 na 21 Julai
2016.
Majina ya waombaji waliochaguliwa
kwa kila kozi itolewayo na chuo husika yamekabidhiwa vyuoni kupitia Mfumo wa
Udahili wa Pamoja (CAS).
Waombaji waliochaguliwa nao
wamearifiwa kupitia kurasa (profile) zao binafsi au kwa kubofya hapa. Waombaji ambao hawakuchaguliwa
wamejulishwa sababu zilizowafanya wasichaguliwe kupitia kurasa (profile) zao
pia.
Kwa waombaji wa Shahada ya Kwanza
waliowasilisha maombi yao kupitia NACTE, Baraza linapenda kuwaarifu kuwa, mashauriano
kati ya NACTE na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) yanaendelea kufanyika ili
kufanikisha udahili wa waombaji wa kozi za Shahada ya Kwanza kama Serikali
ilivyoagiza.
Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji
NACTE
Tarehe: 22 Julai, 2016 .
|
Saturday, July 23, 2016
Home
HABARI
TAARIFA KWA UMMA:-Kuhusu Kufunguliwa Kwa Mfumo Wa Udahili Wa Pamoja (CAS) Unaoratibiwa na NACTE .
TAARIFA KWA UMMA:-Kuhusu Kufunguliwa Kwa Mfumo Wa Udahili Wa Pamoja (CAS) Unaoratibiwa na NACTE .
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment