IFAHAMU:- Kunywa Maji la Limao kama una Matatizo Kati ya haya. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, July 21, 2016

IFAHAMU:- Kunywa Maji la Limao kama una Matatizo Kati ya haya.


Ukinywa glasi moja ya maji ya uvuguvugu yenye LIMAO katika tumbo tupu ni zaidi ya maji katika mwili wako.

Ina manufaa sana kwa afya zetu. Limao lina vitamin C, B, antioxidant, phosphorus, protein, flavonoids, volatile oils, carbohydrates na potassium.

Mchanyanyiko huu wa limao na maji ni kinga dhidi ya bacteria, kupambana dhidi ya virusi, kuongeza mfumo wa kinga ya mwili, na ina tabia ya kukinga dhidi ya maambukizi. Hii ni kutokana na kuwa limao lina  pectin, magnesium, bioflavonoids, vitamins,limonene, citric acid, na calcium.



Kwa hiyo glasi moja ya limao inasaidia katika digestion, inasaidia kutoa nje maji ya ziada na sumu mwilini, na pia inatibu tatizo la kuongezeka uzito kwa haraka. Na pia ina mazingira fulani yenye alkaline, ambayo inasaidia kusawazisha pH katika mwili.

Maji ya uvuguvugu ya limao yana manufaa haya katika afya zako:

1.Inaongeza kinga ya mwili.
 
Kinywaji hiki huongeza mfumo wa lymphatic na kuufanya ufanye kazi kwa ufanisi.Mfumo wa lymphatic unafanya kazi sambamba
na mfumo wa kinga ya mwili kwa lengo la kulinda mwili.

2.Uondoa mawe kwenye figo.
 
Kutokana na kiwango kikubwa cha potassium, limao linaongeza kiwango cha citrate katika mkojo, na inazuia utengenezaji
wa oxalate.

3.Inatibu Mafua na Homa.
 
Mara zote limao linatumika kupambana na mafua pamoja na Homa. Wingi wa antioxidants na vitamin C katika limao, linasaidia kupambana na bacteria na virusi.

4.Inapunguza maumivu ya joint, na kuvimba.
 
Maji ya limao yanapunguza uric acid katika joints, ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kuvimba.(hasa kwenye arthritis)

5.Inarekebisha uwiano(colitis).
 
Colitis ni hali ya kutokuwa na uwiano sawa kati ya alkaline na acid. Glasi moja ya limao kwa kila siku itasaidia kuweka uwiano sawa kati ya acid na alkaline katika mwili. Na itashusha wingi wa acid katika mwili.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad