CAF KOMBE LA SHIRIKISHO:-Matokeo ya 3-1 yamehitimisha rasmi safari ya Young Africans kuelekea nusu fainali. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, July 26, 2016

CAF KOMBE LA SHIRIKISHO:-Matokeo ya 3-1 yamehitimisha rasmi safari ya Young Africans kuelekea nusu fainali.

Yanga SC imeendelea kuboronga katika mechi za Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika baada ya jioni ya leo,July 26, 2016 kufungwa mabao 3-1 na wenyeji Medeama FC Uwanja wa Essipong Sports mjini Sekondi-Takoradi, Ghana.

Huo unakuwa mchezo wa nne mfululizo Yanga inacheza bila kushinda, ikifungwa mara tatu na kutoa sare moja.

Mabao ya Medeama yalifungwa na Daniel Amoah dakika ya saba aliyemalizia kona ya Enock Atta Agyei na Abbas Mohammed mawili dakika ya 23 na 37, wakati la Yanga lilifungwa na Simon Msuva dakika ya 25 kwa penalti baada ya Obrey Chirwa kuangushwa kwenye boksi.

Na Yanga ingepigwa 4-1 kama si kipa Deo Munishi ‘Dida’ kupangua mkwaju wa penalti  Malik Akowuah dakika ya 10.

Matokeo hayo yanamaanisha Yanga inaondoka kwenye mbio za kuwania Nusu Fainali na sasa inacheza kukamilisha ratiba.

TP Mazembe inaendelea kuongoza Kundi A kwa pointi zake saba, ikifuatiwa na MO Bejaia na Medeama ambazo zote kila moja ina popinti tano, wakati Yanga ina pointi moja.  

TP Mazembe watakuwa wenyeji wa Bejaia kesho, July 27,2016 Lubumbashi wakihitimisha raundi za nne.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad