KLABU BINGWA ULAYA 2015/2016:-Atletico Madrid waenda Fainali wakimsubiri Mshindi kati ya Real Madrid na Manchester City. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, May 04, 2016

KLABU BINGWA ULAYA 2015/2016:-Atletico Madrid waenda Fainali wakimsubiri Mshindi kati ya Real Madrid na Manchester City.

Timu ya  Bayern Munich ya Ujerumani ,wakiwa kwao Allianza Arena Mjini Munich jana May 03,2016 wameifunga Atletico Madrid ya Hispania mabao 2 -1 katika Mechi ya Pili ya Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Ulaya lakini wametupwa nje kwa Bao la Ugenini na Atletico Madrd kutinga Fainali.

Wiki iliyopita huko Vicente Calderon Jijini Madrid Atletico Madrd walishinda 1- 0 na hivyo Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili  kuwa magoli 2-2 lakini Bao la Atletico Madrid katika kipigo chao cha 2-1 huko Allianz Arena limewanufaisha kwa kuhesabika Mawili.
Katika Mechi hii ya Marudiano, Bayern walitangulia kufunga kwa Frikiki ya Xabi Alonso na kisha katika Dakika ya 34 Thomas Muller wa Bayern akakosa Penati iliyochezwa na Kipa Jan Oblak.

Kisha Antoine Griezmann akaisawazishia Atletico lakini Robert Lewandowski akaipa Bayern uongozi wa Bao 2-1 kwa Bao la Kichwa na Atletico kukosa Penati iliyopigwa na Fernando Torres katika Dakika ya 84.
Atletico Madrid wanatinga Fainali ya Klabu Ulaya huku mara mbili wakikosa Taji baada ya Kufungwa na Bayern Mwaka 1974 na Miaka Miwili iliyopita kutwangwa na Mahasimu wao Real Madrid.

Kwenye Fainali ya Mwaka huu itakayochezwa huko San Siro Mjini Milan, Italy hapo Mei 28,2016, Atletico Madrid  watacheza na Mshindi kati ya Real Madrid na Manchester City wanaorudiana Leo ,May 4, 2016,Usiku wakiwa 0-0 kutoka Mechi ya Kwanza.
Kipa wa Atletico Madrid, Jan Oblak akiokoa mkwaju wa penalti wa mshambuliaji wa Bayern Munich, Thomas Muller katika mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumanne ,May 03, 2016,Uwanja wa Allianz Arena mjini Munich. 

Penalti hiyo ilitolewa baada ya Jose Gimenez kumchezea rafu Javi Martinez .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad