MATOKEO / RATIBA LA LIGA 2015/2016:- Jumamosi Aprili 23,2016 - Atletico de Madrid ,FC Barcelona na Real Madrid Zatoboa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, April 24, 2016

MATOKEO / RATIBA LA LIGA 2015/2016:- Jumamosi Aprili 23,2016 - Atletico de Madrid ,FC Barcelona na Real Madrid Zatoboa.

Mshambuliaji wa Barcelona, Luis Suarez (kushoto) sambamba na Wachezaji wenzake wakifurahia ushindi wao katika mchezo wa La Liga usiku jana April 23,2016 Uwanja wa Nou Camp. 

Mabingwa hao Watetezi na Vinara wa La Liga ,Barcelona waliitandika Sporting Gijon ,kwa magoli 6-0 huku Luis Suarez akipiga Bao 4 na hii ni mara yake ya pili mfululizo kupiga Bao 4 kwenye Mechi.

 Suarez pia alifunga Bao 4 Jumatano, wakati Barcelona wanaimimina Deportivo La Coruna magoli 8-0.
Karim Benzema akizungumza na kocha wa Real Madrid, Mfaransa mwenzake Zinedine Zidane baada ya kushindwa kuendelea na mchezo Jumamosi April 23,2016 wakati alipoumia goti lake la kulia, na sasa anawaachia hofu mashabiki wa timu yake kuelekea Nusu Fainali ya Kwanza ya michuano ya Ulaya Uwanja wa Etihad katikati ya wiki ijayo.

Mapema Jana , Real Madrid na Atletico Madrid walishinda Mechi zao za La Liga na kwa Matokeo hayo yamewaweka Barcelona kwenye uongozi wa La Liga wakiwa na Pointi 82 sawa na Atletico Madrid lakini wao wako juu kwa ubora wa magoli huku Real Madrid wakiwa Nafasi ya 3 Pointi kwa Pointi 81 huku Mechi zikibaki 3 tu Ligi kumaliza msimu wake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad