TUMBUA MAJIPU:-Tanzania yafichua wizi wa milioni 700. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, February 11, 2016

TUMBUA MAJIPU:-Tanzania yafichua wizi wa milioni 700.

Shirika la ndege la Air Tanzania.

Serikali ya Tanzania imebaini wizi wa takribani shilingi milioni 700 ,katika Shirika lake la Ndege (ATCL) kupitia kampuni ya wakala wa ukatishaji tiketi ya Salama World Travel iliyopo visiwa vya Comoro.

Hii ni moja ya harakati za Serikali kulifufua Shirika la Ndege Tanzania.

Kufuatia upotevu huo wa fedha, mkurugenzi wa Fedha wa ATCL,Bw Steven Kasubi amesimamishwa kazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Prof.Makame Mbarawa.

 Akizungumza na waandishi wa habari ,Jana February 10,2016,jijini Dar es Salaam ,Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa ameeleza kuwa  wizi huo umefanywa kwa kushirikiana na wafanyakazi wa shirika hilo.

Kufuatia upotevu huo Serikali  imechukua hatua thabiti ikiwemo kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Fedha wa ATCL Bw.Steven Kasubi ili kupisha uchunguzi utakaofanywa na kikosi  cha polisi  kitengo cha usalama mtandaoni  ili kubaini mtandao mzima uliohusika  ” alisema Prof.Mbarawa.

Vilevile aliongeza kuwa Serikali imemuagiza  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) kufanya uchunguzi kwa mawakala wengine wote wa Shirika hilo kubaini kama fedha za uuzaji wa tiketi hizo zinarudishwa kama inavyotakiwa.

Prof.Mbarawa ametoa wito kwa wananchi kuachana na wizi kwa  njia ya mtandao kwa kuwa sheria ya mtandao iliyoanzishwa mwaka jana inatumika katika kuhakikisha kuwa watuhumiwa wanafikishwa katika mkondo wa sheria na kuchukuliwa hatua stahiki.

 
Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari  kwa WhatsApp +255789925630 Or +255756830214.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad