TASWIRA PICHA:- PPF Wakabidhiwa rasmi Jengo Jipya la Ghorofa 10 lenye thamani ya Bilioni 32.5 –Arusha. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, February 07, 2016

TASWIRA PICHA:- PPF Wakabidhiwa rasmi Jengo Jipya la Ghorofa 10 lenye thamani ya Bilioni 32.5 –Arusha.

Sehemu ya muonekano wa mbele wa jingo la PPF.

Jengo hilo maalumu kwa shughuli za ofisi na biashara lenye ghorofa 10 sambamba na eneo la basmenet yenye uwezo wa kupaki magari 168, lina thamani ya shilingi bilioni 32.5. Limejengwa eneo la Corridor, Kitalu Na. 15 Barabara ya zamani ya Old Moshi Jijini Arusha. lina huduma zote muhimu kwa majengo ya kisasa zikiwemo 'lifti' za kutosha, majenereta makubwa, mataki ya maji na mafuta ya jenereta, mfumo wa kukabiliana na moto na bila kusahau camera 90 za usalama na eneo kubwa la kuegesha magari ndani ya jengo.

Kwa mujibu wa Mbunifu na Msimamizi Mkuu wa mradi huo wa kisasa, Arch Mawala, ujenzi wa jengo hilo ulianza rasmi Agosti 2 mwaka 2008 ukitarajiwa kukamilika miezi 104 baadae na ulikamilika rasmi (practica completion) mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka jana,2015. 

Hata hivyo imewachukua miaka miwili na miezi 3 kuweza kukamilisha kila kitu katika ubora wa kiwango cha juu, ambapo miezi hiyo mitatu ni ya nyongeza ya muda kutokana na sababu ambazo hazikuweza kuzuilika.

Mpaka kufikia kukabidhiwa kwake hii leo, tayari ukaguzi wa mamlaka za Jiji na Usalama wa Majengo umeshakamilika na ruhusa ya matumizi kutolewa.
 
Tayari jengo hilo limeshapata wapangaji watatu ambao wapo kwenye jengo tayari zikiwemo benki za TIB na FBNB, huku asilimia 21 ya wapangaji wengine wakiwa wamekwisha saini mikataba na PPF na wapangaji wengine 24 wakiwa katika mazungumzo.
Kiongozi Mkuu wa mfuko wa PPF (Director General) William Erio (kushoto) akipokea michoro ya jengo jipya la PPF Jijini Arusha kutoka kwa Mbunifu na Msimamizi Mkuu wa mradi wa ujenzi wa jengo hilo,  Arch. Dudley Mawalla (kulia) kutoka kampuni ya   MD Consultancy Ltd ya Dar es Salaam, katika hafla fupi ya makabidhiano rasmi ya jengo kutoka kwa mkadarasi wa kichina CREJ (EA) Ltd. Anayeshuhudia Katikati ni Injinia wa Miradi ya PPF, Injinia Marko Kapinga.
Kiongozi mkuu wa Kampuni ya CRJE (EA) Ltd, Bw Hu Bo (kulia) ambaye kamapuni yake ndio ilikuwa mkandarasi mkuu wa mradi akikabidhi funguo kwa Director General wa PPF Bw William Erio kama ishara ya makabdihiano ramsi ya jengo la PPF Plaza la Jijini Arusha hii leo. Kwa mbali anashuhudia Meneja wa jengo hilo kutoka PPF .
DG William Erio katika picha ya pamoja mbeye ya sehemu kuu ya kuingilia kwenye jengo akiwa na timu ya wakandarasi, wasimamizi wabunifu wa mradi pamoja na wataalamu kutoka PPF Dar es Salaam.HABARI NA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.


Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari  kwa WhatsApp +255789925630 Or+255756830214.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad