EPL 2015/2016:-Timu ya Leicester City, Leo February 06,2016 yaibonda Timu ya Pili Manchester City Bao 3-0. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, February 06, 2016

EPL 2015/2016:-Timu ya Leicester City, Leo February 06,2016 yaibonda Timu ya Pili Manchester City Bao 3-0.


Timu ya Leicester City, Leo February 06,2016 wameibonda Timu ya Pili Manchester City Bao 3-1 kwenye  Uwanjani  wa Etihad Stadium na kupaa kileleni mwa Ligi wakiwa Pointi 6 mbele.

Magoli mawili ya Beki Robert Huth na moja la Riyad Mahrez ndizo ziliiua Manchester City huku Sergio Aguero akiipa City Bao lao pekee.


Mbali ya kuifunga Timu ya 3 ,Tottenham kwao White Hart Lane Mwezi Januari, ushindi huu wa Leo umeonyesha wazi kuwa sasa Leicester wanao uwezo kuwa Mabingwa wa England tofauti na dhana ya wengi kuwa watateleza.

Mechi ijayo kwa Leicester ni huko Emirates hapo Februari 13 dhidi ya Arsenal.

Kwa matokeo hayo vijana wa Claudio Ranieri wanaendelea kuongoza ligi wakiwa na pointi 53 wakifuatiwa na City ambao wanabaki na pointi zao 47.



Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari  kwa WhatsApp +255789925630/+255756830214.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad