AJALI / PICHA:-Ndege ya kijeshi yaua ''100'' Indonesia - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, June 30, 2015

AJALI / PICHA:-Ndege ya kijeshi yaua ''100'' Indonesia

Vikosi vya usalama vikiwa kazini.   

Ndege ya Uchukuzi ya Jeshi la Anga la nchini Indonesia imeanguka eneo la Medan, Kaskazini mwa Jimbo la Sumatra mapema leo June 30,2015.

 



Takriban watu 100 wameuawa baada ya ndege ya uchukuzi wa kijeshi ya Indonesia kuanguka mapema leo katika maeneo yenye makazi ya watu huko Medan Sumatra.

Maafisa wa kijeshi wanasema kuwa tayari miili 49 imepatikana katika eneo la ajali.

Maafisa wa kijeshi nchini Indonesia, wanasema kwamba ndege hiyo ya uchukuzi ya majeshi ya taifa hilo, ilianguka muda mfupi baada ya kupaa angani.

Ndege hiyo ya kubeba mizigo aina ya Hercules 130 ilikuwa na wahudumu 12 na abiria 113 ilipoanguka.

Afisa mkuu wa jeshi la wanahewa Air Marshall Agus Supriatna amesema kuwa hakuna manusura waliopatikana hai.

Kuna ripoti kuwa watu bado wanasikika wakipiga mayowe katika majengo yaliyoanguka.
Sehemu ya mabaki ya ndege hiyo.

Shughuli za uokoaji zikiendelea katika eneo la tukio.

Kuna ripoti kuwa watu bado wanasikika wakipiga mayowe katika majengo yaliyoanguka.

Ndege hiyo iliharibu nyumba baada ya kuanguka katika mji wa Medan, kaskazini mwa Jimbo la Sumatra.

Picha za runinga zilizorekodiwa wakati ndege hiyo ilipokuwa ikianguka na zile za kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha moto unatoka kwenye mabaki ya ndege hiyo.

Msemaji wa Jeshi la Anga nchini Indonesia amesema kuwa, rubani alikuwa ameomba kurejea katika uwanja wa kambi ya kijeshi kwa sababu ya matatizo ya kimitambo.

Source:- BBC Swahili.

 Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad