VURUGU IRINGA:-Tazama Picha 10 za yaliyojili Mjini Ilula Leo Februari 24,2015 wakati Wananchi wakifunga Barabara Kuu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, February 24, 2015

VURUGU IRINGA:-Tazama Picha 10 za yaliyojili Mjini Ilula Leo Februari 24,2015 wakati Wananchi wakifunga Barabara Kuu.

Muonekano wa Kituo cha Polisi cha mji wa Ilula mkoani Iringa baada ya Wananchi  wenye hasira mjini Ilula, mkoani Iringa,  kuvamia kituo cha Polisi na kuvunja milango kisha kuwafungulia mahabusu waliokuwemo ndani, wakachoma moto baadhi ya magari yaliyokuwepo kituoni hapo pamoja na mafaili Leo Februari 24,2015 ,Majira ya Asubuhi.
Muonekano wa mji wa Ilula mkoani Iringa baada ya wananchi kufunga barabara kuu ya mji huo leo Februari 24,2015.
Mabasi ya kwenda mikoani yakiwa yamepaki baada ya wananchi kufunga barabara.

Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, tukio hilo limetokea leo asubuhi kufuatia mwanamke ambaye hakufahamika jina lake kujigonga ukutani na kuanguka kisha kufariki dunia wakati akiwakimbia Polisi waliokuwa kwenye oparesheni ya kuwakamata watu wanaokunywa pombe wakati wa asubuhi.

Habari zaidi zinapasha kwamba, licha ya kuchoma moto magari, waliziba barabara kuu ya kwenda mikoani na kuyazuia magari kupita,  hali iliyosababisha Polisi kuwakabili lakini walizidiwa nguvu na kuingia ndani ya basi la Nyagawa.

Askari wakiwa ndani ya gari hilo waliendelea kushambuliwa na wananchi kwa mawe na kuvunja vioo vyake na habari zinasema wananchi kadhaa wamejeruhiwa katika kadhia hiyo.




Muonekano wa mji wa Ilula mkoani Iringa baada ya wananchi kufunga barabara kuu ya mji huo leo Februari 24,2015.

Picha zote kwa hisani ya Mitandao ya Kijamii....UNGANA  NASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad