LIGI KUU TANZANIA 2014/2015:-Haya ndio Matokeo ya Mechi Viporo vya leo Februari 19,2015 - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, February 19, 2015

LIGI KUU TANZANIA 2014/2015:-Haya ndio Matokeo ya Mechi Viporo vya leo Februari 19,2015

Yanga SC hii Leo Februari 19,2015 wakiwa huko Sokoine Jijini Mbeya wamechukua usukani wa Ligi Kuu Vodacom baada ya kuitandika Tanzania Prisons Bao 3-0 wakati waliokuwa Vinara, Azam FC, ambao pia ndio Mabingwa Watetezi, kutoka Sare 0-0 na Ruvu Shooting huko Mabatini, Mlandizi, Mkoa wa Pwani.

 Yanga SC sasa wapo kileleni wakiwa Pointi 2 mbele ya Azam FC huku Timu hizo zikiwa zote zimecheza Mechi 14 kila mmoja.

Bao za Yanga zilifungwa na Simon Msuva, Bao 2, na Mbrazil Coutinho aliepiga Bao 1 lakini yeye ndie Nyota wa Gemu baada ya kutengenezai Bao zote 2 za Msuva alieunganisha Kona zake mbili Dakika za 3 na 62.

Bao la Coutinho lilifungwa Dakika ya 11 na kusindikizwa wavuni na Beki wa Prisons katika harakati za kuokoa lakini Bao hilo linabaki kwa Mbrazil huyo kwa vile Mpira huo hata kama Beki huyo asingeugusa ulikuwa unatinga tu.

 Hizi Mechi za Leo ni za viporo kwa Yanga SC na Azam FC na wote watatinga tena dimbani Jumapili kwa Yanga SC kubaki huko huko Sokoine Mbeya kucheza na Mbeya City na Azam FC kuwa kwao Azam Complex, Chamazi, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam kucheza na Tanzania Prisons.

Jumapili wiki endi hii  ipo Mechi moja zaidi huko Kambarage, Mjini Shinyanga, wakati Stand United itakapoikaribisha Simba huku , Jumamosi zipo Mechi 3 za Ligi huko Miji ya Shinyanga, Mtwara na Tanga.

UNGANA  NASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

RATIBA VPL 2014/2015.

Jumamosi Februari 21,2015.

Kagera Sugar v Polisi Moro

Ndanda v Coastal Union

Mgambo Shooting v Mtibwa Sugar

Jumapili Februari 22,2015.

Mbeya City v Yanga

Stand United v Simba

Azam FC v Tanzania Prisons

MSIMAMO VPL 2014/2015.

NA
TIMU
P
W
D
L
F
 A
 
GD
PTS
1
Yanga
14
8
4
2
18
7
 
11
28
2
Azam FC
14
7
5
2
22
12
 
10
26
3
Kagera Sugar
15
5
6
4
12
11
 
1
21
4
Simba
14
4
8
2
15
11
 
4
20
5
Ruvu Shooting
15
5
5
5
10
11
 
-1
20
6
Mtibwa Sugar
14
4
7
3
15
14
 
1
19
7
Coastal Union
15
4
7
4
10
9
 
1
19
8
JKT Ruvu
15
5
4
6
14
15
 
-1
19
9
Polisi Moro
15
4
7
4
12
13
 
-1
19
10
Mbeya City
14
4
5
5
9
11
 
-2
17
11
Ndanda FC
15
4
4
7
13
18
 
-5
16
12
Stand United
15
3
6
6
13
18
 
-5
15
13
Mgambo JKT
13
4
2
7
7
51
 
-8
14
14
Tanzania Prisons
14
1
8
5
10
15
 
-5
11

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad