CHIDI BENZ HURU:-Ni baada ya ya kulipa faini ya 900,000/= kwa kukutwa na madawa ya kulevya. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, February 27, 2015

CHIDI BENZ HURU:-Ni baada ya ya kulipa faini ya 900,000/= kwa kukutwa na madawa ya kulevya.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Jana Februari 26,2015, imemwachia mwana muziki wa Hip Hop Nchini Tanzania, Rashid Makwiro 'Chid Benz' baada ya kulipa faini ya sh. 900,000 kufuatia kukamatwa akiwa na madawa ya kulevya.

Chid Benz alikamatwa mwaka jana 2014 katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa na madawa ya kulevya, ikiwemo misokoto ya bangi.

Mwanamuziki huyo ambaye alikiri kosa hilo wiki iliyopita, alikamatwa uwanjani hapo akiwa anajitayarisha kupanda ndege kwenda mkoani Mbeya kwenye tamasha la muziki, akipatikana na hatia ya makosa matatu ikiwemo kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin yenye thamani ya sh. 38,638, bangi ya sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae.


UNGANA  NASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad